Home Kimataifa Ronaldinho na wachezaji wengine 5 waliowahi kupewa heshima hii Santiago Bernabeu 

Ronaldinho na wachezaji wengine 5 waliowahi kupewa heshima hii Santiago Bernabeu 

806
0
SHARE

Andres Iniesta alionyesha moja ya mchezo mzuri sana ambao utakumbukwa kwa muda mrefu juzi katika dimba la Santiago Bernabeu – wakati FC Barcelona ikiinyosha Real Madrid 4-0. Iniesta alikuwa nahodha wa Barca kwa mara ya kwanza katika historia ya El Clasico.

Hii ilikuwa ndio mara ya kwanza kufunga na kutoa assist katika mechi moja ya EL Clasico.

Wakati Munir alipoingia badala ya Iniesta katika dakika ya 77 minutes, mashabiki wa Real Madrid waliinuka kutoka kwenye viti vyao na kumpigia makofi mchezaji huyo wa mahasimu wao.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa mashabiki wa Real madrid kuonyesha heshima ya namna hiyo kwa wachezaji wa timu pinzani, na hapo chini ni listi ya wachezaji 6 waliowahi kupata heshima hiyo.

1. Andres Iniesta, Barcelona. 2015.

2. Ronaldinho – Barcelona. 2005.

Kiungo huyu wa kibrazil alikuwa katika kilele cha kiwango chake wakati Barca walipoinyoosha Madrid 0-3, na kiwango kikubwa alichoonyeaha Ronaldinho kiliwafanya mashabiki wa Los Blancos kusimama na kushangilia moja ya magoli bora kabisa ya Dinho katika maisha yake ya soka.

3. Diego Maradona, Barcelona. 1983.

Mmoja wanasoka bora zaidi kuwahi kutokea duniani aliwasimamisha mashabiki wa Real Madrid wakati alipofunga goli zuri la uwezo binafsi akiwa Na Barca katika El Clasico.

4. Del Piero, Juventus. 2008.

Italian maestro alikuwa mfalme wa Bernabeu wakati alipoifunga Madrid mara mbili katika mchezo wa mtoano wa ligi ya mabingwa wa ulaya.

5. Andrea Pirlo, Juventus. 2015.

 Pirlo alipata heshima ya mashabikiaa Madrid ndani ya Bernabeu katika nusu fainali ya Champions League msimu uliopita baada ya kuwa na mchezo mzuri sana.
 6. Fernando Morientes, Monaco. 2004.

Morientes alikuwa Monaco kwa mkopo akitokea Real Madrid wakati alipofunga goli zuri la kichwa vs  Real Madrid katika mchezo ambao Los Blancos walikufa 2-4 katika dimba la Santiago Bernabeu- mchezo huo ulipomalizika mashabiki wa Madrid walisimama na kumpigia makofi Morientes.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here