Home Kimataifa RAMOS, MARCELO WAOMBA KUSAMEHEWA MADRID

RAMOS, MARCELO WAOMBA KUSAMEHEWA MADRID

402
0
SHARE

Ramos 4

Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos na mlinzi mwenza, Marcelo wamewaomba mashabiki wa klabu yao ya Madrid kuwasamehe kutokana na kipigo cha magoli 4-0 walichokipokea toka kwa mahasimu wao Fc Barcelona katika uwanja wa Santiago Bernabeu, mjini Madrid mwishoni mwa juma hili.

Ramos anasema, “kama wachezaji, tunaomba radhi sana kwa mashabiki wetu kwa kilichotokea. Tunajua vitendo vina nguvu kuliko Maneno, hivyo tunahitaji kuonesha uwanjani na kuwafariji mashabiki”.

Aidha mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Mbrazil Marcelo amesema hawakupoteza mchezo kwa sababu ya ‘attitude’ huku wakisisitiza kuwa morali iko juu na kwamba wanamuamini kocha wao Rafael Benitez ambaye hii ilikua ni El Classico yake ya kwanza.

Akiunga mkono kauli hiyo ya Marcelo, kiungo Luka Modric amesisitiza imani waliyonayo wachezaji kwa mwalimu wao Rafael Benitez, huku akikazia kuwa attitude yao kama wachezaji iko vizuri.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here