Home Kimataifa OKLAHOMA CITY THUNDER YAZINDUKA NA KUWATUNGUA DALLAS MAVERICKS. WESTBROOK ON FIRE

OKLAHOMA CITY THUNDER YAZINDUKA NA KUWATUNGUA DALLAS MAVERICKS. WESTBROOK ON FIRE

486
0
SHARE

okc

Kama umepitwa na game hii usikubali kupitwa tena na game nyingiza za NBA kwasababu Startimes wana suluhisho lako, ukiwa na king’amuzi cha Startimes utaona channel ya NBA TV ambapo kuna content ya NBA masaa 24.

Westbrook alikuwa na pointi 31 na pasi 11 , akafunga  vikapu viwili muhimu katika sekunde 63 za mwisho, na Oklahoma City Thunder wakatoka nyuma kwa pointi nyingi  katika robo tatu na kwenda  kushinda ushindi mgumu wa 117-114  na kuvunja mwendelezo wa kushinda michezo sita mfululizo wa Dallas Mavericks.

Serge Ibaka alikuwa na pointi 16, rebounds tisa na na kupiga block muhimu kabisa ya sekunde za mwisho  kwa Oklahoma City . Thunder ilikuwa bila nyota wake aliye nje kutokana na majeraha,  Kevin Durant kwa mchezo wa sita mfululizo. Oklahoma City imeshuhudia rekodi ya  3-3 akiwa hayupo.

Wachezaji watano wengine wa  Oklahoma City walifunga katika tarakimu mbili yaani zaidi ya pointi 10, ikiwemo Serge  Ibaka , Dion Waitersi (14) , Anthony Morrow (14) , Enes Kanter (12) na Nick Collison (10).

Deron Williams aliiongoza  Dallas kwa pointi 20, huku pia akikosa mtupo muhimu zikiwa zimebaki sekunde 8.4. Wesley Matthews alimaliza na pointi 18 , wakati Pachulia alikuwa na pointi 12 na 10 rebounds.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here