Home Kimataifa BALE ATAREJEA TENA EPL? MWENYEWE ATOA MSIMAMO WAKE JU YA HILO

BALE ATAREJEA TENA EPL? MWENYEWE ATOA MSIMAMO WAKE JU YA HILO

499
0
SHARE

Bale

Nyota wa Real Madrid Gareth Bale ameshindwa kukanusha taarifa za kurejea kunako ligi kuu Uingereza lakini akisisitiza bado anafuraha kubwa kuendelea kubaki Santiago Bernabeu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales amekuwa akihusishwa na klabu ya Manchester United mwisho wa mwaka jana licha ya kujiunga na miamba hiyo ya Uhispania mwaka 2013.

Bale amesema kwamba “kamwe hawezi kusema kamwe” kuhusu kurejea kwake ligi kuu Uingereza, licha ya kupewa nafasi ya kucheza katikati na kocha wake Rafa Benitez na kumfanya awe na furaha klabuni hapo.

“Mipango yangu wakati nilipoanza kucheza mpira ilikuwa ni kufikia malengo yangu–na Real Madrid ndio kilele chenyewe,” alinukuliwa na Daily Mirror.

“Sasa nipo hapa na, nataka kushinda mataji mengi zaidi, ninafanya kila liwezekanalo kuhakikisha napata mafanikio.

“Siwezi kusema haiwezekani kwangu kurudi ligi kuu Uingereza, kwa sababu huwezi kujua nini kitatokea. Nina furaha sana hapa”.

“Nilikuwa na mazungumzo mafupi na Rafa wakati wa majira ya joto na nimefurahishwa kwamba nitapata nafasi kubwa ya kucheza msimu huu,” aliongeza.

“Napenda kucheza nyuma ya mshambuliaji na nahisi hiyo ndio nafasi yangu. Naweza kuzunguka sehemu mbalimbali uwanjani na, ninapopata mpira nikiwa katika nafasi nzuri basi naweza kushambulia. Hii ni nafasi nzuri sana kwangu na mwaka huu utakuwa mzuri sana kwangu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here