Home Kimataifa BAADA YA KUUA UGENINI, KLOPP ATAKA KUWAPA RAHA ANFIELD

BAADA YA KUUA UGENINI, KLOPP ATAKA KUWAPA RAHA ANFIELD

533
0
SHARE

Jurgen

Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool amesema atafarijika zaidi kama atapata ushindi mkubwa kama alioupata dhidi ya Manchester City ugenini, katika uwanja wa nyumbani wa Liverpool Anfield na kuwapa raha mashabiki wake.

Tangu atue Liverpool majuma kadhaa yaliyopita, Jurgen Klopp amekua na rekodi nzuri zaidi katika mechi za ugenini ambapo aliweza kuwafunga Chelsea kwa goli 3-1 Stamford Bridge, akawafunga Manchester City 4-0 katika uwanja wa Etihad huku pia akitoa sare ugenini dhidi ya Tottenham Hotspur, pamoja na kushinda ugenini katika michuano ya Uropa ligi.

Wachambuzi nchini England wanaona ili Liverpool ipate chochote msimu huu wanahitaji kuhamishia fomu ya mechi za ugenini katika uwanja wao wa nyumbani ili kuvuna chochote msimu huu.

Jurgen 1

Tayari kocha Jurgen Klopp ameshasema mipango yake ya kukiongezea mbinu na morali kikosi hicho ili kipate matokeo katika uwanja wa nyumbani wa Anfield na kuwapa raha mashabiki.

Akiongelea kuhusu mbio za ubingwa Klopp amesema michuano ya Ulaya (champions league) ndio ya muhimu zaidi na kwamba ndio pesa iliko. Anasema itakua ngumu lakini wanahitaji kujitahidi kufanya kitu ili kuona itakuaje mwisho wa msimu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here