Home Kimataifa BAADA YA KIPIGO KUTOKA BARCELONA, BENZEMA AJIKUTA PEKEAKE MAZOEZINI

BAADA YA KIPIGO KUTOKA BARCELONA, BENZEMA AJIKUTA PEKEAKE MAZOEZINI

513
0
SHARE

Benzema 2

Mshambuliaji Karim Benzema jana Jumapili alitokea pekee kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Madrid kufanya mazoezi baada ya kocha Rafael Benitez kuwapa ofa ya mapumziko wachezaji wa kikosi cha kwanza siku ya Jumapili kutokana na kipigo cha goli 4-0 kutokana kwa mahasimu wao Barcelona.

Benzema 3

Karim Benzema aliamua pamoja na kupewa ofa ya kupumzika, kutokea mazoezini huku akifanya mazoezi na kikosi cha pili sanjari na baadhi ya wachezaji wakubwa kama Arbeloa.

Benzema 1

Real Madrid ilipokea kipigo hicho kikubwa kutoka kwa Barcelona cha mabao 4-0 magoli yakifungwa na Luis Suarez (2), Neymar pamoja na Iniesta.

Mechi hii ilikua ni ya kwanza ya El Classico kwa kocha Rafael Benitez huku akitakiwa kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Shaktar Donestic Jumanne hii huku wachezaji wakianza mazoezi Jumatatu hii.

Benzema

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here