Home Ligi EPL Aguero, Tevez, Suarez katika Listi ya Wafungaji Bora EPL kutoka Amerika Kusini

Aguero, Tevez, Suarez katika Listi ya Wafungaji Bora EPL kutoka Amerika Kusini

1025
0
SHARE

Kipigo cha jumamosi iliyopita kutoka kwa Liverpool ni kitu ambacho watu wengi katika klabu ya Manchester City  lakini ilikuwa ni siku ya kumbukumbu nzuri kwa mmoja wa wachezaji wa Manuel Pellegrini. 

  Goli la Sergio Aguero katika dimba la Etihad vs Liverpool lilimfanya atimize jumla ya magoli 7 katika mechi 9 za Premier League msimu huu. 

  Goli hilo pia alilofunga katika dakika ya 44 likamfanya mshambuliaji huyo kuwa mwanasoka mwenye asili ya Amerika ya kusini ambaye anaongoza kwa kufunga magoli mengi zaidi katika ligi kuu ya Uingereza. 

Mshambuliaji huyo mwenye umri miaka 27, sasa ana magoli 85 katika EPL – goli moja zaidi ya muargentina mwenzie Carlos Tevez ambaye wakati akivichezea vilabu vya West Ham, Man United na Man City alifanikiwa kufinga magoli 84.

 

Luis Suarez ni watatu kwenye listi hiyo akiwa na magoli 69 aliyoyafunga katika misimu mitatu na nusu aliyoichezea Liverpool kabla ya kuhamia FC Barcelona 2014. 

 
Mruguay mwenzie Suarez, Gus poyet anashika nafasi ya 4 katika kidti hiyo akiwa na magoli 54 aliyoyafunga wakati akiwa katika safu ya kiungo ya vilabu vya Chelsea Na Tottenham.  
 Nolberto Solano anakamilisha listi ya tano ya wafungaji bora wa muda wote wa kutoka America ya kusini katika EPL – Solano alivitumikia vilabu vya Newcastle, Aston Villa na West Ham.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here