Home Ligi EPL USINGIZI WA DEPAY VIPI, NDO UMEISHA? MANCHESTER UNITED YAWA MCHARO

USINGIZI WA DEPAY VIPI, NDO UMEISHA? MANCHESTER UNITED YAWA MCHARO

503
0
SHARE

DEPAYTroy Deeney akaenda kutoka shujaa mpaka kuwa mhanga  katika muda wa dakika tano baada ya mshambuliaji huyo wa Watford  kufunga penalti na kisha kujifunga na kutoa mwanya kwa Manchester United kupata ushindi wa 2-1 katika uwanja wa Vicarage Road.

Watford ilionekana kuwa itapata walau pointi moja baada ya Deeney mnamo dakika ya 87 kufunga goli kwa njia ya  mkwaju wa penati na kufuta uongozi wa mapema baada ya goli la Memphis Depay.

Haikudumu sana baada ya nahodha huyu wa  Hornets kujikuta akiweka kimiani mpira wa Bastian Schweinsteiger muda mfupi baadaye na kutoa nafasi kwa upande wa Louis van Gaal kubeba pointi tatu.

Kwa ushindi huu maana yake Manchester United mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote katika michezo nane iliyopita ya mashindano yote. Hii inaendelea kumuweka Van Gaal katika nafasi nzuri ya kujibu wale wote waliokuwa wanampinga dhidi ya aina yake ya mchezo kwa klabu ya United.

Ilikuwa na maana kwamba ilikuwa ni mchezo wa kwanza  wa ligi kwa Depay kuanza tangu United ilipoadhibiwa kwa mabao 3-0 kutoka kwa Arsenal Oktoba 4 huku vijana Marcus Rashford na Sean Goss waliokuwa wakizungumzwa sana hatimaye waliitwa kikosini na kuwepo kwenye benchi.

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here