Home Ligi EPL SASA NI LIVERPOOL FIRMINO+COUTINHO SIO LIVERPOOL FC. LIVERPOOL YAIUA MAN CITY ETIHAD,...

SASA NI LIVERPOOL FIRMINO+COUTINHO SIO LIVERPOOL FC. LIVERPOOL YAIUA MAN CITY ETIHAD, STERLING KIMYA KIREFU

856
0
SHARE

LIVERPOOL

LIVER

Liverpool waliistua  Manchester City kwa mabao matatu kipindi cha kwanza kwenye Uwanja wa Etihad na kupata ushindi wa 4-1 dhidi ya klabu ya Manuel Pellegrini ambao wameondolewa katika nafasi ya kwanza ya kugombea taji la ligi kuu ya Uingereza.

Eliaquim Mangala alifungua akaunti ya magoli kwa kufunga kwenye lango lake  mwenyewe  mnamo dakika saba kipindi cha kwanza.

manga

Katika khali inayoonekana Klopp kuelekea kupata ubora wa wachezaji wake wabunifu  wakibrazil, Philippe Coutinho na Roberto Firmino baada ya muunganiko wao kupelekea nyongeza ya mabao kufikia 3 katika dakika 32.

COU

Sergio Aguero alionyesha kuwa ni mshambuliaji bora baada ya kufunga goli zuri kabisa kwa juhudi zake binafsi  dakika chache kabla ya mapumziko huku  upande wa Manuel Pellegrini ukijaribu kujikusanya na kurejea mchezoni.

ag

Uharibifu ulikuwa tayari umeshafanyika kwa kiasi kikubwa huku Martin Skrtel akifunga mahesabu kwa kukwamisha wavuni mpira wa shuti kali katika dakika za miwsho na kuondoa matumaini ya Man City kurejea juu katika msimamo na kuitoa Leicester  City .

SKR

Klopp alianza na kikosi ambacho wachambuzi wengi walistuka kutokana na kutokuwepo straika wa asili na kumuanzisha Firmino huku wachezaji kama Benteke na Sturridge wakianzia katika benchi.

Liverpool walionekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa hasa wakizima mashambulizi ya Man City yaliyokuwa yanaonekana kuanzishwa kwa kutokea katikati na muda mwingi counter attacks ndio ilikuwa silaha yao na kuwalazimu city kufanya makosa kadhaa.

Hata hivyo Man City walionekana kwa kiasi kikubwa kumkosa nahodha wao Vincent Kompany kwani kulikuwa na kutokuelewana baina ya Mangala na Deminichelis na muda mwingi sehemu ya ulinzi ilikosa kiongozi.

STERLING VS LIVERPOOL?

Moja ya mambo yaliyokuwa yanasubiriwa kwa hamu ilikuwa ni mpambano waSterling dhidi ya klabu yake ya zamani ya Liverpool ambayo hakuondoka vizuri. Haukuwa mchezo mzuri kwake hasa ukizingatia fomu aliyokuwa nayo katika siku za karibuni yeye na Kevin Debryune.

Na pengine nafasi bora aliyoipata ilikuja dakika ya 65 lakini akajaribu kutokuwa mchoyo kwa kutaka kumpa Aguero afunge lakini Mignlolet alikuwa katika eneo sahihi kuokoa.

sterlin

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here