Home Kimataifa Ronaldo vs Bale – Nani aliye-flop kumzidi mwenzie katika EL Clasico

Ronaldo vs Bale – Nani aliye-flop kumzidi mwenzie katika EL Clasico

861
0
SHARE

 Usiku wa jana ulikuwa ni wa aibu kwa Real Madrid na mashabiki wao, huku mastaa wao Gareth Bale na Cristiano Ronaldo wakishindwa kufanya lolote la maana kuizuia Barcelona kupata ushindi mkubwa zaidi katika dimba la Bernabeu tangu walipoifunga Madrid 6-2 chini ya utawala wa Ronaldinho, Eto’o na Henry.

Wachezaji hao ghali zaidi duniani jana walikuwa na siku mbaya zaidi katika historia yao ya kucheza EL Clasico – lakini mmoja wao alikuwa flop zaidi ya mwenzie. Mtandao wa takwimu za masuala ya michezo wa Opta umetoa takwimu zao za mechi ya jana dhidi ya vijana wa Luis Enrique na zipo kama ifuatavyo:

TAKWIMU ZA GARETH BALE VS BARCELONA
Katika mechi ya jana winga huyu wa Welsh aligusa mpira mara 41 tu, akitengeneza nafasi 3, akapiga krosi 5 na kati hizo ni krosi moja tu ndio iliyomfikia mlengwa – alipambana kushinda mpira kwa asilimia 25 tu dhidi ya wachezaji wa timu pinzani.

 TAKWIMU ZA CRISTIANO RONALDO VS BARCELONA
Mwanasoka bora wa dunia (mpaka January 2016) usiku wa El Clasico aligusa mpira mara 46, akafanikiwa kutengeneza nafasi 1, akapiga krosi 1 ambayo haikufanikiwa – lakini akashinda vita dhidi ya wapinzani kwa asilimia 53.
TAKWIMU ZA JUMLA 
Wawili hawa ambao wote kwa pamoja waliigharimu Madrid kiasi cha £166m – walicheza dakika 90 kila mmoja – Bale alipiga pasi 23, Ronaldo 29 – usahihi wa pasi ulikuwa asilimia 73 kwa Bale na asilimia 89 kwa Ronaldo – Bale alipiga mashuti 2 na Ronaldo 2, mashuti yaliyolenga goli – Bale 1, Ronaldo yote mawili yalilenga goli kipa akaokoa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here