Home Kimataifa MASHABIKI WA MADRID WAMFANYIA KITU INIESTA KAMA RONALDINHO

MASHABIKI WA MADRID WAMFANYIA KITU INIESTA KAMA RONALDINHO

800
0
SHARE

Iniesta 6

Mchezaji nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Andres Iniesta jana usiku aliweka rekodi aliyoiweka Ronaldinho Gaucho mwaka 2005 baada ya mashabiki wa Real Madrid kusimama kumshangilia mchezaji huyo kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji hao waliouonesha na kusababisha kupigiwa saluti na mashabiki wa mahasimu wao wa Bernabeu.

Iniesta 7

Andres Iniesta jana alikua katika ubora wa juu dhidi ya Real Madrid, akitoa pasi ya goli la pili iliyomkuta Neymar ambaye hakufanya kosa, lakini katika ubora zaidi Iniesta alifunga pia goli na kuisaidia timu yake ya Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 4-0 katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Iniesta 8

Hali kama hiyo iliwahi kumtokea Ronaldinho Gaucho mwaka 2005 alipoisaidia Barcelona kuifunga Real Madrid magoli 3-0 katika uwanja wa Santiago Bernabeu na kuwasimamisha mashabiki wa Real Madrid kumshangilia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here