Home Ligi EPL MAJERUHI YAZIDI KUIANDAMA ARSENAL, SASA WAFIKIA 8

MAJERUHI YAZIDI KUIANDAMA ARSENAL, SASA WAFIKIA 8

694
0
SHARE

Francis Coquelin

Hali si shwari Emirates, makao makuu ya klabu ya Arsenal ambapo hadi jana Francis Conquelin na Mikel Arteta walitoka uwanjani wameumia na kusababisha idadi ya majeruhi klabuni hapo kufikia wanane.

Arsenal tayari inawakosa Jack Wilshere, Aaron Ramsey, Danny Welbeck, Theo Walcott na Oxlade Chamberlain kwa majeruhi na sasa inakabiriwa na wimbi kubwa la majeruhi huku wakijiandaa na mechi dhidi ya Dinamo Zagreb Jumanne hii mechi ambayo lazima washinde ili kujipa matumaini ya kusonga mbele katika michuano ya klabu barani Ulaya.

Hakuna taarifa za haraka kujua ni lini nani atarudi kikosini huku kocha Arsene Wenger akihaha kuhakikisha anapata matokeo katika hali yeyote ile.

Tayari athari za majeruhi zinaweza kuwa zimeanza kujitokeza kwani Arsenal tayari jana jioni walipoteza mechi kwa kipigo cha magoli 2-1 toka kwa Westbromwich Albion katika mchezo wa ligi kuu nchini England na kushuka kutoka nafasi ya pili hadi ya nne.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here