Home Kimataifa KRISTAPS PORZINGIS ANAENDELEA “KUWAPROVE WRONG WATU” KATIKA KKIWANGO BORA KABISA AWAADHIBU HOUSTON...

KRISTAPS PORZINGIS ANAENDELEA “KUWAPROVE WRONG WATU” KATIKA KKIWANGO BORA KABISA AWAADHIBU HOUSTON ROCKETS

435
0
SHARE

POR

Carmelo Anthony na Derek Fisher wameendelea  kusisitiza kuwa walijua miezi kadhaa iliyopita kwamba Kristaps Porzingis alikuwa na uwezo wa aina hii ya utendaji na kiuchezaji.

Porzingis alikuwa na pointi 24, 14 rebounds na alifanikiwa kublock shots 7 huku akiiongoza New York Knicks  kuibuka na ushindi 107-102 dhidi  ya wazee wa makombora wa Houston yaani Houston Rockets alfajiri ya leo jumapili.

PORZ

Anthony muda mrefukidogo  uliopita alihusishwa na kuwa miongoni mwa wale waliokasirishwa na kitendo cha Pjil Jackson kumchagua mchezaji huyu katika draft ya mwaka huu katika namba nne.

Hii yote ilitokana na wengi kuaini kuwa alihitaji muda mrefu sana sana kuja kuwa mchezaji wa kariba ya juu, huku Knicks wakihitaji mtu wa maana kwa muda huo.

“Ilikuwa ni wasiwasi kutoka kwa watu ambao hawakujua ,” Anthony alisema. “Watu hawakujua nini cha kutarajia. Hakuna mtu aliyewahi kumwona kabla na watu wote walikuwa hivyo na kuchukizwa kwamba  Knicks ilijiandaa kumchukua na baadae kuondoka naye.”

Porzingis anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri wa miaka 20 kuweka namba ama takwimu za aian hii mgongoni kwake katika mchezo mmoja tangu mchezaji Shaquille O’Neal afanye hivyo katika msimu wa 1992-1993.

“Najua kwa ukweli kwamba ilikuwa ni jambo moja kwamba aliruka kutoka kwenye  menejimenti na kwa Phil ( Jackson ) kwamba alikuwa mtu sahihi na kweli anavutia kuhusu mchezo wake lakini kikubwa zaidi juu uwezo wake wa kuzuia,” kocha wake Fisher Derek alisema.

New York Knicks imeshinda mchezo wake wa nne mfululizo na pia kuondoa uteja mbele ya Houston Rockets. Kabla ya mchezo huu, Knicks walikuwa wamepoteza michezo 10 mfululizo mbele ya Houston.

Pia lazima wafurahie matokeo yao ya msimu huu kwani ushindi wa nane msimu uliopita waliupata wakiwa na rekodi ya 8-26. James Harden alikuwa na pointi 24, pasi 10 na rebounds saba kwa Houston waliopoteza kwa mara ya sita katika mechi yao za mwisho saba.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here