Home Ligi EPL Kauli ya Van Gaal juu ya kumrudisha Ronaldo Old Trafford msimu ujao.

Kauli ya Van Gaal juu ya kumrudisha Ronaldo Old Trafford msimu ujao.

701
0
SHARE

Baada ya tetesi za muda mrefu sana kuhusu kurudi nyumbani kwa mtoto kipenzi wa Old Trafford – Cristiano Ronaldo, hatimaye kocha wa United Louis Van Gaal ametoa kauli ambayo itawafurahisha mashabiki wengi wa United.

 Kumekuwepo na taarifa siku za hivi karibuni kwamba Ronaldo ambaye jana alicheza kwenye mechi ya kipigo cha 4-0 vs Barcelona – kwamba ataondoka Madrid mwishoni mwa msimu huu.

Van Gaal hivi karibuni alizungumzia kuhusu usajili anaotaka kuufanya katika kuimarisha kikosi chake na Mdachi huyo ameonekana kuwa na matumaini ya kufanya kazi na Ronaldo.

“Anacheza upande wa winga na ana kasi sana, pia anafunga magoli. Sidhani kama kuna kocha duniani ambaye hapendi kuwa naye kikosini,” Van Gaal amekaririwa kwenye magazeti ya leo ya UK.

 “Ni kweli tunajaribu kusajili wachezaji wazuri wakubwa na sio Ronaldo pekee yake, lakini sio rahisi kuwapata aina hii ya wachezaji.

“Tusubiri tukiendelea kutumaini.”

Ronaldo, 30, ana mkataba na Madrid mpaka 2018, japokuwa kwa sasa hali inazidi kuonyesha wazi mshambuliaji huyo ataihama Madrid mwishoni mwa msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here