Home Kimataifa GOLDEN STATE WARRIORS WAITEKA NBA, HAIJAJULIKANA WATAFUNGWA LINI. WAZUNGU WANASEMA THEY ARE...

GOLDEN STATE WARRIORS WAITEKA NBA, HAIJAJULIKANA WATAFUNGWA LINI. WAZUNGU WANASEMA THEY ARE ON FIRE

442
0
SHARE

curry

golden

Rekodi ya  Golden State  Warriors  inaendelea bila kikomo, wakati huu mabingwa watetezi hawa wakipenya kwa kuwalipua timu ngumu ya  Chicago Bulls kwa pointi  106-94 siku ya Ijumaa usiku . Golden State warriors  sasa waweka rekodi ya  14-0 , na wanaelekea katika rekodi bora amayo pengine wataiweka katika NBA ( 16-0 ).

Rekodi za kushinda michezo mingi mfululizo tangu ufunguzi kwa vilabu vyote hata waiokuwa mabingwa watetezi
Rekodi za kushinda michezo mingi mfululizo tangu ufunguzi kwa vilabu vyote hata wasiokuwa mabingwa watetezi

 

Wapiganaji (Warriors)  wanataka rekodi hiyo. Hawana kukana tena na kule  kujifanya kwamba hawana habari hakupo tena. Ubingwa  ni lengo la mwisho, lakini alama nyingine ya historia ambayo ipo karibu sana na inapatiakanika ni ujinga  kupuuza.

Rekodi ya kuanza msimu kwa vilabu vilivyokuwa mabingwa watetezi
Rekodi ya kuanza msimu kwa vilabu vilivyokuwa mabingwa watetezi

“Hiyo rekodi sasa ipo jirani sana, na kiukweli ni lengo la kweli hapa kwa sasa, na ni kitu sisi pia tungependa kukiweka na kuwa watu ambao tutatajwa daima kuwahi kukifanya,” Stephen Curry alisema baada ya mchezo.

Wakati huo huo, ligi ana tatizo . Neno “ndogo”  ndio tatizo, lakini ni dogo linaloendelea kuwa kubwa kila kukicha na pia kila siku. Wakati warriors wakibadilika kila mwisho wa mchezo kwa kuwatoa big mens na kuingiza wachezaji wenye kimo cha kawaida imeendelea kuvitesa vilabu pinzani.

Hiyo imepelekea kupatikana kwa majina ya utani kadha kwa kikosi cha mwisho wa kila mchezo kinachohusisha majina ya  Curry – Klay Thompson – Andre Iguodala – Harrison Barnes – Draymond Green  “Death Lineup (kikosi cha mauaji),”  “Nuclear Lineup (kikosi cha nyuklia),”  “The Closer, (wafunga mahesabu)”.

Na kama vile haitoshi kwa  heshima ya kocha wa muda Luke Walton , wameitwa  ” Knockout Punch (Konde la Knockout). K wa kikosi hiki Golden State Warrriors imeweka rekodi ya kipekee kwa kuwafunga wapinzani kwa rekodiya pointi 74 katika dakika 54 pekee.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here