Home Kimataifa CAVALIERS YAWATAFUNA MWEWE WA ATLANTA. KEVIN LOVE AREJEA KATIKA UBORA CLEVELAND IKIIRARUA...

CAVALIERS YAWATAFUNA MWEWE WA ATLANTA. KEVIN LOVE AREJEA KATIKA UBORA CLEVELAND IKIIRARUA ATLANTA HAWKS.

438
0
SHARE

LOV
 Kevin Love alifunga  pointi 25 ambazo ni nyingi zaidi kwake msimu huu, LeBron James aliongeza 19  na Cavaliers ikawapiga Atlanta Hawks 109-97 siku ya Jumamosi usiku ikiwa ni alfajiri ya jumapili kwa huku Tanzania.

Ikumbukwe kuwa timu hizi mbili ndizo zilizokutana katika hatua ya fainali ya kanda ya mashariki msimu uliopita na Atlanta kuambulia kichapo kibaya cha michezo minne bila majibu.

” Hadi kufikia hatua hii ni kweli khali imeendelea kuwa nzuri na yenye kupendeza kiasi kwa upande wetu, ” alisema kocha David Blatt a. “Tatizo letu kubwa mpaka sasa ni  kuwa tunawakosa wachezaji wengi sana.”

“Pia jambo la kushangaza ni kuwa wachezaji wetu wengi muhimu hawapo kutookana na majeraha lakini ni vyema kuwa hawa waliopo wamekuwa wakiibuka na kufanya kazi tarajiwa na katika khali bora, ambalo ndilo la muhimu zaidi. ”

Guard Mo Williams (kifundo cha mguu ) amekosa michezo miwili iliyopita na Centre wao  Timofey Mozgov (bega la  kulia) anaweza kukaa nje kwa takribani  wiki mbili. Kyrie Irving ( goti ) na Iman Shumpert (upasuaji mkono wa kulia ) bado hawajaweza kucheza kabisa  msimu huu.

Kevin Love  na Lebron  James wote walikuwa na  rebounds 11 . JR Smith alifunga pointi 15 huku Tristan Thompson akidaka rebounds 16 ambazo ni nyingi zaidi kwake kwa msimu huu.

Kyle Korver na Paul Millsap wote walimaliza na pointi 14 kwa timu yao ya Atlanta Hawks, ambayo imepoteza michezo minne kati ya mitano.

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here