Home Ligi EPL RAHEEM STERLING KUIADHIBU LIVERPOOL LEO?

RAHEEM STERLING KUIADHIBU LIVERPOOL LEO?

509
0
SHARE

Starling

Na Simon Chimbo

Klabu za Liverpool na Manchester City leo zinakutana katika mchezo wa ligi juu nchini England katika mechi inayotarajiwa kuwa Kali na ya kusisimua katika uwanja wa Etihad mjini Manchester saa 20:30 kwa saa za Afrika mashariki huku gumzo likiwa ni jinsi wachezaji Raheem Sterling na James Miller watakavyocheza dhidi ya timu zao za zamani.

James Milner aliyekua akiichezea Manchester City kwa misimu kadhaa yuko Liverpool hivi sasa na kwamba itakua ni mara yake ya kwanza kurudi Etihad akiwa mchezaji wa timu pinzani, sijui ataweza kiasi gani kukabiliana na hisia dhidi ya timu yake ya zamani huku pia hisia za mashabiki zikitarajiwa kuonekana dhidi yake.

Starling 3

Lakini pamoja na James Milner katika mchezo huu ni trela ambapo Raheem Sterling ndio picha kamili kutokana na gumzo na utata mkubwa uliotawala wakati wa usajili wake mwezi Julai msimu huu na kupelekea hasira kubwa kwa mashabiki wake wa Liverpool huku kocha Brendan Rodgers akipambana kumbakisha bila mafanikio.

Bila shaka uwezo na kipaji cha kijana huyu ndiyo shida kubwa iliyosababisha yatokee yote yaliyotokea wakati wa usajili wake. Sababu za kocha Brendan Rodgers kumng’ang’ania asiondoke na hata kumuachia baada ya dau kuwa ni kubwa mno (pauni milioni 49) ilikua ni uthibitisho wa kipaji na uwezo wa Raheem Sterling na hapo hasira za mashabiki wa Liverpool ambao bila shaka leo watajaribu kumtoa mchezoni kwa kumzomea kila atakapokua na mpira.

Starling 1

Lakini City leo inaweza kuiadhibu Liverpool kama tu mabeki wa Liverpool watataka kukomaa na Raheem pekee na kuwapa faida Kelvin De Bruins na Sergio Kun Aguero ambaye anarejea leo kuwadhuru. Lakini pia kutokana na Raheem kuyajua madhaifu ya walinzi wa zamani wa Liverpool inaweza kuwa hatari zaidi kwa Liverpool ambao watakua ugenini.

Kitu tofauti hapa leo ni namna kocha mpya wa Liverpool Jurgen Klopp alivyoibadilisha sana Liverpool, wamekua pamoja, morali uko juu, ni kitu pekee Liverpool watatakiwa kuwa nacho huku wakitegemea wachezaji kama Coutinho kuwa katika fomu ya hali ya juu sanjari na uwezo wa Benteke na Daniel Sturridge katika safu ya ushambuliaji.

Starling 2

Manchester City watamuhitaji Otamendi mlinzi wao wa kati kutoka Valencia ambaye yupo katika fomu yake ya juu kuzuia washambuliaji aina ya Benteke na Daniel Sturridge huku akina Fernando na Fernandinho wakitakiwa kumdhibiti sana Philippe Coutinho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here