Home Ligi EPL MEMPHIS DEPAY SASA KAZI KWAKO MAN UNITED

MEMPHIS DEPAY SASA KAZI KWAKO MAN UNITED

582
0
SHARE

Depay 2

Baada ya kutopangwa tangu mara ya mwisho alipocheza na kutolewa wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Arsenal, Memphis Depay sasa anatarajiwa kuongoza mashambulizi ya Manchester United mara baada ya majeruhi kuikabili klabu huyo.

Manchester United inakabiliwa na majeruhi katika safu ya mshambuliaji ambapo Wayne Rooney ambaye anaumwa, Anthony Martial aliumia wakati timu ya taifa ikicheza Jumanne hii na Maruane Fellaini wote wako nje leo United ikisafiri kuikabili Watford majira ya saa 15:45 alasiri.

Memphis Depay anayetarajiwa kupangwa leo kuongoza mashambulizi, anakabiliwa na mtihani mkubwa hii leo kuonesha alichonacho kwenye pocket kutokana na kukalia benchi tangu mwezi September mwaka huu.

Van Gaal akimzungumzia Depay anasema ni kipaji ambacho anaamini kulingana na muda atakua sawa na kwamba tatizo la vijana wengi ni consistency ambapo Depay anatakiwa kuonesha uwezo wake hii leo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here