Home Kimataifa KUELEKEA MCHEZO WA EL CLASICO, FAHAMU TAKWIMU MBALIMBALI ZA MIAMBA HIYO YA...

KUELEKEA MCHEZO WA EL CLASICO, FAHAMU TAKWIMU MBALIMBALI ZA MIAMBA HIYO YA SOKA LA HISPANIA

518
0
SHARE

barca-madrid

Real Madrid leo usiku itakuwa mwenyeji wa FC Barcelona kwenye pambano la kwanza la El Clasico msimu huu kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.

Rafa Benitez atakuwa anakiongoza kikosi cha Madrid kwenye mchezo wa El Clasico kwa mara ya kwanza huku kikosi chake kikiwa nyuma ya Barcelona kwa pointi tatu kwenye msimamo wa La Liga.

Real Madrid walipokea kichapo kwa mara ya kwanza chini ya kocha wao mpya Rafa Benitez kwenye mchezo uliopita dhidi ya Sevilla kabla ya mapumziko kupisha ratiba ya mechi za kimataifa za kalenda ya FIFA.

Luis Suarez na Neymar wamekuwa tishio kwenye safu ya ushambuliaji ya Barcelona licha ya kukosekana kwa Lionel Messi, lakini mkali huyo wa Argentina anaweza kurejea kwenye mchezo huo baada ya kuwa nje kwa muda kufuatia kuumia goti na kukaa nje ya uwanja kwa miezi miwili.

Hapa unaweza kuangalia takwimu mbalimbali za miamba hii ya soka nchini Hispania kabla ya mchezo wa leo kupigwa.

Real Madrid vs Barcelona-takwimu

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here