Home Ligi EPL STURRIDGE SASA MAMBO SAFI LIVERPOOL

STURRIDGE SASA MAMBO SAFI LIVERPOOL

594
0
SHARE

Sturridge

Mshambuliaji Daniel Sturridge wa Liverpool amejitangaza kuwa yuko fiti na sasa anatarajiwa kurudi uwanjani mara baada ya kuwa ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza na wachezaji wenzie wa Liverpool.

Sturridge ambaye hajakuwa sawa kwa kipindi cha takribani miezi 18 kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, amerudi tena upya na anahitaji kutoumia na kufanya kazi ili kujiweka sawa kwa kocha mpya mjerumani Jurgen Klopp.

Sturridge 1

Akizungumza katika hafla za uzinduzi wa mavazi ya klabu akiwa kama mgeni mualikwa, Sturridge amesifia impact ya kocha mpya Jurgen Klopp klabuni hapo huku akisema anaona ni wakati mahsusi kwake na kwa klabu.

Liverpool hivi sasa imekua ikimtumia mshambuliaji raia wa Ubelgiji Christian Benteke pekee na kwamba Daniel Sturridge ana kazi ya kufanya pia kupambana na ukiacha Benteke, lakini pia Origi ambaye pia anaonekana kupata nafasi kwa kocha Jurgen Klopp.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here