Home Kimataifa MESSI AONESHA VIATU MAALUM ATAKAVYOVAA KATIKA MECHI YA ‘EL CLASSICO’

MESSI AONESHA VIATU MAALUM ATAKAVYOVAA KATIKA MECHI YA ‘EL CLASSICO’

605
0
SHARE

messi 2Zimebaki siku mbili tu kabla ya mchezo unaosubiliwa kwa hamu na wapenzi wengi wa soka duniani kupigwa kati ya Real Madrid na Barcelona katika uwanja wa Bernabeu.
Ni kiu ya wadau wengi wa soka hasa mashabiki wa Barcelona kujua kama mshambuliaji wao hatari Lionel Messi atacheza katika pambano hilo.

Messi alionekana juzi katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya Barcelona akifanya mazoezi na taarifa za kitabibu toka klabu ya Barcelona zinasema kuwa nyota huyo anaweza kucheza mechi hiyo ingawa ni mapema kuwa na uhakika wa asilimia 100.

Lionel-Messi-3Lakini Messi mwenyewe anaonekana kuwa tayari kucheza mchezo huo na ameonesha viatu maalum vilivyotengenezwa na kampuni ya Adidas kwa jaili ya mchezo wa ‘EL Classico’ siku ya Jumamosi.

messi 1Viatu hivyo vimepambwa na rangi nyeusi,kijani na nyekundu.
Messi hajacheza mchezo wowote tangu alipoumia katika mchezo dhidi ya Las Palmas mnamo mwezi wa tisa mwaka huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here