Home Kimataifa LAKERS YALAMBISHWA ARDHI TENA. BRANDON KNIGHT KATIKA KIWANGO CHA MAISHA YAKE

LAKERS YALAMBISHWA ARDHI TENA. BRANDON KNIGHT KATIKA KIWANGO CHA MAISHA YAKE

565
0
SHARE

knightBrandon Knight aliweza kupata trible double yake ya kwanza ya maisha ya Basketball katika NBA dhidi ya klabu ya Los Angeles Lakers alfajiri a leo. Brandon Knight aliisadia klabu yake ya Phoenix Suns kuibuka na ushindi wa 120-101 .

Brandon Knight alifunga point 30, akamaliza na pasi 15 na Rebound 10. Eric Bledsoe aliongeza pointi 21 na Warren alifunga pointi 19 kwa Suns ambazo ni nyingi zaidi katika maisha yake ya NBA.

“Walikuja juu katika robo ya nne na kuamua kuwa walikuwa wanakwenda kuchukua walichotakiwa kuchukua ambacho ni ushindi ,” alisema Lou  Williams wa LA Lakers . ” Ninahisi hatukuwa tukifanya kitu kimoja kama wao.”

Kwa ujumla, Suns waliwashinda Lakers 21-8 baada  ya muda wa 05:40 katika robo ya nne na kuongoza kwa  103-86, kabla ya kupanua wigo wa uongozi  kwa pointi nyingi kama 21 katika dakika za mwisho.

“Muunganiko  kwa timu hii ni mzuri sasa hivi ,” alisema kocha wa  Suns Jeff Hornacek , ambaye timuyake  imeshinda michezo yake mitatu iliyopita kwa jumla ya pointi 57 .

“Wamekuwa wakipongezana kwa pamoja na kufurahia wote. Dalili nzuri kwa kocha kuona ni wote wakisaidiana kwa namna tofauti kwa  kila mmoja.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here