Home Ligi EPL FABREGAS HAJUI NINI TATIZO LA CHELSEA MSIMU HUU

FABREGAS HAJUI NINI TATIZO LA CHELSEA MSIMU HUU

610
0
SHARE

Fabregas

Kiungo Cesc Fabregas wa Chelsea na timu ya taifa ya Hispania amesema msimu huu kwao umekua mbaya sana na kwamba hajui nini kinaenda vibaya katika kikosi hicho cha kocha Jose Mourinho.

Akiongea kwa uchungu sana, Cesc ameonesha kukasirishwa sana na jinsi msimu unavyoenda huku akisema matokeo hayawatendei haki kwani wanacheza vizuri kuliko matokeo wanayopata uwanjani.

Fabregas ambaye wiki mbili zilizopita alikaririwa akisema wachezaji wote wako nyuma ya kocha wao ameendelea kusisitiza kuwa ana mahusiano mazuri na kocha wake Jose Mourinho tofauti na taarifa zisizo rasmi mtaani kwamba wawili hao hawako sawa.

Msimu huu ni mbaya zaidi katika historia ya Chelsea kwa miaka mingi na mbaya zaidi kwa kocha Jose Mourinho ambapo hadi sasa klabu hiyo inashika nafasi ya 16 na ikiwa na pointi 11 katika michezo 12 iliyochezwa hadi sasa msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here