Home Kitaifa WATANZANIA WASIWEKEZE KILA KITU KWA MBWANA SAMATTA, THOMAS ULIMWENGU

WATANZANIA WASIWEKEZE KILA KITU KWA MBWANA SAMATTA, THOMAS ULIMWENGU

877
0
SHARE
Mbwana Samatta (kushoto) pamoja na Thomas Ulimwengu (kulia)
Mbwana Samatta (kushoto) pamoja na Thomas Ulimwengu (kulia)
Mbwana Samatta (kushoto) pamoja na Thomas Ulimwengu (kulia)

Na Shaffih Dauda, Dar es Salaam

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo Jumamosi itawakabili timu namba mbili  kwa ubora barani Afrika, timu ya Taifa ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa raundi ya mtoano kuwania nafasi ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya fainali za kombe la dunia-Kanda ya Afrika.

Stars inatoka katika kambi ya wiki moja na siku kadhaa nchini Afrika Kusini itawakabili ‘Mbweha wa Jangwani’ baada ya kufuzu hatua ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1 dhidi ya Malawi mwezi uliopita.

Kwa mara ya kwanza Stars itaingia uwanjani kucheza na timu bora zaidi Afrika ikiwa na mfungaji bora wa ligi ya mabingwa Afrika, namzungumzia kijana wa miaka 22, Mbwana Samatta.

Sina shaka kuhusu uwezo wa Samatta ambaye nilimshuhudia Jumapili iliyopita akiipa ubingwa wa Afrika upande wa vilabu timu ya TP Mazembe ya DR Congo.

Sitazungumzia sana mechi yenyewe lakini ningependa kuwaambia Watanzania wenzangu kuwa hatupaswi kuamini moja kwa moja katika uwezo wa mchezaji mmoja au wawili katika timu na ili kuishinda Algeria wachezaji wote kuanzia kwa golikipa hadi mchezaji wa mwisho katika safu ya ushambuliaji wanapaswa kucheza katika kiwango cha kufanana.

Samatta anazungukwa na nahodha wa timu ya taifa ya Zambia ambayo Jumatano hii iliifunga Sudan 1-0 jijini, Khartoom. Namzungumzia kiungo mshambuliaji Rainford Kalaba, pembeni ya Samatta pale TP Mazembe anacheza na mchezaji pekee wa timu ya Taifa ya Ivory Coast anayecheza barani Afrika, Roger Assale, Mghana, Solomon Asante, n.k

Kiujumla, Samatta anazungukwa na ‘rundo’ la wachezaji wenye vipaji ambao wanajituma sana ndani ya uwanja kwa muda wote wa mchezo. Huduma ambayo ‘Samagoal’ amekuwa akiitoa klabuni kwake ni tofauti kidogo na ile ambayo Watanzania wamekuwa wakitaraji kutoka kwa mchezaji huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji 10 bora wanaocheza ndani ya Afrika kwa mwaka huu wa 2015.

Kwa nini Samatta wa TP Mazembe ni tofauti na huyu anayeichezea Stars? Ubora wake ni uleule, tofauti ni kwamba, akiwa TP anakutana na wachezaji wenye vipaji kama yeye ambao pia hucheza kwa nidhamu, kujituma na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

Mafanikio ya Samatta na ‘patna’ wake Thomas Ulimwengu ndani ya klabu yao wiki iliyopita ni ya ‘mfanowe’. Ni wachezaji wa kwanza wa Kitanzania kucheza mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Afrika. Katika michezo miwili ya fainali kati ya TP Mazembe na USM Algers ya Algeria, Samatta amefanikiwa kufunga magoli mawili kati ya manne ya TP na kutengeneza goli lingine moja.

Ushindi wao wa taji la mabingwa Afrika umewafanya Watanzania wengi kujenga imani kwamba, Stars inaweza kuishinda na kuitoa Algeria! Kila kitu kinawezekana katika mchezo wa soka, lakini ukitazama aina ya wapinzani ambao tunakwenda kucheza nao ni sawa na ‘mlima mrefu’ ambo tunapaswa kuupandaa.

Ulimwengu anacheza kwa kupambana sana akiwa klabuni kwake TP Mazembe na amekuwa akicheza hivyo hivyo hadi timu ya Taifa Stars. Lakini Samatta anahitaji ‘muunganiko’, anahitaji wachezaji wenzake wacheze kwa asilimia ya juu. Anahitaji wachezaji ambao wana uwezo wa kuusoma mchezo. Kila Mtanzania ukimuuliza hivi sasa kwanini anaamini Stars itashinda dhidi ya Algeria anakwambia “Mbwana Samatta”.

Lakini mchezo wa mpira wa miguu si kama mchezo wa ngumi au tenis, mtu anapambana mwenyewe. Akiwa mzuri anapata matokeo. Lakini mchezo wa mpira wa miguu unahitaji sana uwezo wa kiuchezaji wa mchezaji mwingine. Ukitaka kuuona uwezo halisi wa Samatta katika timu ya Taifa ni lazima, Shomari Kapombe, Nadir Haroub, Kelvin Yondan, Ally Mustapha wote wacheze inavyotakiwa katika idara zao.

Timu ambayo Samatta aliifunga magoli mawili katika fainali ya CAF Champions league haina hata mchezaji mmoja katika timu ya Taifa ya Algeria! Inamaanisha kuwa wanategemea zaidi mkusanyiko wa wachezaji wao wanaofanya vizuri barani Ulaya. Algeria ina wachezaji wanaofanya vizuri katika ligi kuu England, Hispania, Ureno na kwingineko.

Algeria wamekuja na ‘timu kabambe’, Rais M’Bolhi (Antalyaspor/Uturuki), Azzedine Doukha (JS Kabylie), Malik Asselah (CR Belouizdad). Viungo: Mehdi Zeffane (Rennes/Ufaransa), Mohamed Khoutir Ziti (JS Kabylie), Faouzi Ghoulam (Napoli/Italia), Djamel Mesbah (Sampdoria/Italia), Carl Medjani (Trabzonspor/Uturuki),Aïssa Mandi (Reims/Ufaransa), ukweli itakuwa mechi ngumu kwa Stars kuliko Algeria.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here