Kikosi cha Ujerumani kimetolewa kwenye hotel moja huko Ufaransa wakiwa kwenye makazi yao kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya ufaransa kutokana na kusambaa kwa tetesi za kuwepo kwa bomu.
Polisi walifika haraka eneo la tukio na kuwatoa wachezaji wote wa kikosi hicho kwa kutumua magari tofauti. Basi lao la kikosi liliachwa kwa ajili ya ukaguzi chini ya polisi.
Kamanda wa polisi kwenye kituo cha jirani anasema walipata hizo tetesi na wakaamua watu wote pamoja na wachezaji hao watoke ili kupisha uchunguzi ambao ulitumia mbwa na vifaa vingine.
Hadi mwisho hakukupatikana kitu chochote kama bomu lakini kikosi hakuna uhakika wa kikosi hicho kurudi tena kwenye hoteli hiyo.