Home Kimataifa SIRI YA SERBIA KWA MAFANIKIO YA SOKA LA VIJANA; WAO WAMEWEZA...

SIRI YA SERBIA KWA MAFANIKIO YA SOKA LA VIJANA; WAO WAMEWEZA KWANINI TANZANIA TUSHINDWE. KILA WALILOFANYA LINAWEZEKANA TUKIAMUA. TIZAMA NA VIDEO KAMILI

691
0
SHARE

HM

Kwa msaada wa Tovuti ya UEFA na chama cha soka nchini Serbia

Ikiwa na idadi  ndogo ya watu takribani  milioni saba , Serbia haiwezi kuchukuliwa kuwa moja ya mabwawa makubwa  Ulaya yenye utajiri  mkubwa wa vipaji vya  mpira wa miguu au soka. Hata hivyo, timu zake za vijana ni zisizokosekana  katika mashindano ya UEFA  na yale ya Kombe la Dunia.

Na karibuni ni mafanikio yao ya kuchukua ubingwa dunia mwezi Juni kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 yaani u20. Hii inakuja baada ya muendelezo wa  mafanikio ambayo ni yenye tija na  ya kukumbukwa. Timu ya U19 ilishinda taji la Ulaya mwaka 2013 na kufikia nusu fainali mara tatu katika mashindano ya hivi karibuni.

SEBIA

HIVYO, NI NINI HASA SIRI YAO YA MAFANIKIO?

Serbia mara zote ilikuwa ni nchi ya kuzalisha wachezaji bora . Wengi bado mnakumbuka vipindi vya majina mashuhuri kama Dragan Džajić au Dragan ‘ Piksi ‘ Stojkovic katika rangi za Yugoslavia kipindi hicho.

Na ilipotokea kuvunjwa kwa nchi , hata hivyo, mchezo huu  mzuri ulishuka thamani na haukuwa ukivutia kwa vijana wengi. Katika miaka kumi iliyopita , mpira wa miguu na katika hali ya kushangaza  ulishika nafasi ya nne  kwa  umaarufu  wa michezo, na vijana zaidi wakaamua kuelekea  kwenye  mpira wa kikapu, mpira wa wavu na tenisi.

Chama cha Soka cha Serbia ( FSS ) kikaamua kuanza  kwa kampeni ya nchi nzima , ‘ iliyoitwa (My School, My Team), yaani shule yangu – Timu yangu ‘. Hii ilipelekea kurejesha  mashindano ya mpira wa miguu kwa watoto katika shule za msingi na ingawa ilikuja  taratibu lakini kwa hakika imetoa mkondo wa kutosha wa vipaji.

nyumba ya mpira ya serbia,
nyumba ya mpira ya serbia,

FSS kisha  kwa umakini ikaorodhesha mambo muhimu  na hatua kwa hatua kukatekelezwa mbinu bora kutoka mamlaka za jadi ya mpira wa miguu. Mwaka 2007, wakasaini itifaki na Shirikisho la Soka  la Hispania ( RFEF ) ambayo ilihusisha mechi za kirafiki mara kwa mara kwa timu za vijana.

Pamoja na hayo wakakubaliana kubadilishana waamuzi na wafanyakazi wa afya  wakati pia wakashauriwa kwa karibu kufuatilia maendeleo katika baadhi ya idara zinazoheshimika za kuendeleza vijana kimichezo hasa soka ambazo ni idara za Italia na Ufaransa katika Coverciano na Clairefontaine.

Matokeo yake ilipelekea kuanzishwa kwa ‘ Jumba la Soka ‘ (The House Of Football)  kule Stara Pazova mwaka 2011, kituo kinachokidhi viwango vya kisasa kabisa  kikiwa na viwanja saba , ukumbi wa michezo na hoteli . Eneo hilo limekuwa  daima likitumiwa na timu za taifa  za Serbia, ambazo huanza mapema kabisa kwa umri  wa U11.

muonekano wa nje wa house of football
muonekano wa nje wa house of football

Eneo hilo pia liliandaliwa ili kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji pindi chama cha soka cha Serbia FSS, kikihitaji  kuandaa na kuwa mwenyeji wa michezo mara kwa mara ya kimataifa na mashindano  yenye ushindani mkubwa mawili kwa umri sahihi hasa timu  kutoka Yugoslavia ya zamani na Balkans , lakini pia kutoka maeneo mengine ya Ulaya.

FSS pia ina mengi ya ‘ katikati ‘ hasa timu kama vile U16s  na U18s . Lengo ni kutoa kila kizazi cha wachezaji ambacho kitakuwa kichwa na mwanzo mzuri wa kutoa mafunzo ya mwaka mzima kuhusu thamani ya mechi na mafunzo kabla ya kuanza safari yao ya kufuzu katika mashindano rasmi UEFA na kombe la dunia , kama vile U17s na U19s .

ramani na muonekano wa ndani wa house of football
ramani na muonekano wa ndani wa house of football

Mipango ya kufundisha iliyoanzishwa na UEFA , wakati huo huo , imesaidia sana katika kuelimisha na kuchagua makocha ambao wenye  uwezo wa kufanya kazi na timu zao za  taifa husika. Veljko Paunović , kocha  wa U- 20 aliyeshinda Kombe la Dunia , na Radovan Curcic, sasa kocha  mwandamizi wa timu ya taifa, wote  wawili walijitokeza kupitia utaratibu huu.

Bado kumekuwa kuna nafasi ya kuboresha , ingawa, hasa katika miundombinu. FSS inatambua kwamba ili kuzalisha wachezaji wa kiwango cha  juu , wanahitaji kuwa na hali nzuri . Kwa msaada wa mpango wa maendeleo ya soka ulaya yaani UEFA Hattrick  Programme na Serikali za Mitaa , viwanja 12 vya hali ya juu vyenye nyasi bandia vimejengwa nchini kote.

Shirikisho la soka nchini humo  litavisimamia na kuvidumisha , lakini lengo lao ni kutumika kwa  mafunzo na mahitaji ya ushindani wa vilabu vya nchini, nchini humo.

WATANZANIA KUNA GUMU LOLOTE HAPA WALAU NUSU YA HAYA WALIYOFANYA, KAMA WAMEOMBA MSAADA NA WAKAPATA SISI TUNASHINDWA NINI? KAMA WAMETAMANI NA WAKAWEZA, SISI JE? 

HEBU TIZAMA VIDEO YA ENEO NA JUMBA HILO

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here