Home Kimataifa KOBE MAJERUHI, LAKERS YAENDELEA KUPOTEA. YAPIGWA NA ORLANDO MAGIC

KOBE MAJERUHI, LAKERS YAENDELEA KUPOTEA. YAPIGWA NA ORLANDO MAGIC

492
0
SHARE

ORLShabazz Napier aliiongoza  Orlando akiwa na pointi 22, ikiwa ni pamoja na point 3 tano, na Evan Fournier aliongeza 16. Orlando Magic walipata  pointi 65 kutoka katika benchi lao, ikiwa ni pamoja na Vucevic kufunga pointi 18.

Victor Oladipo ambaye ni mfungaji bora wa pili katika klabu ya  Orlando Magic, alitoka kwenye  mchezo katika robo ya kwanza kwa majeraha  na hakurudi.

Nyota wa Lakers  Kobe Bryant hakuwepo mchezoni, amekosa  mchezo wake wa pili mfululizo  kutokana na majeraha ya mgongo. Lakers ikipoteza 99-101

Lakers walisambaza wafungaji wao vyema, na wachezaji sita kufunga zaidi ya pointi kumi, wakiongozwa na Hibbert  aliyekuwa na pointi 15 na D’Angelo Russell alikuwa na 14.

Lou Williams, ambaye alifunga pointi 13, alijaribu katika hatua fulani kuvaa  majukumu ya Kobe kama mwamuzi mchezo katika sekunde za mwisho. Ingawa mpira aliojaribu kufunga katika sekunde za mwisho kupata ushindi uliishia hewani.

“Ni wazi kwamba hatukuweza  kurusha mpira vyema,   na waliskuja na mipango yao ambayo ilifanikiwa kila walipojaribu  na inabidi umpe pongezi kijana huyu mkubwa ( Vucevic ) kwa alichofanya,”  kocha  wa Lakers Byron Scott alisema. “Tulikuwa na siku mbaya kiulinzi kwa sababu kila mara tulianguka.

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here