Home Ligi EPL HII NDIYO KAULI YA CARLO ANCELOTTI KUHUSU CHELSEA

HII NDIYO KAULI YA CARLO ANCELOTTI KUHUSU CHELSEA

562
0
SHARE

Carlo Ancelotti

Kocha wa zamani wa klabu za AC Milan, PSG, Chelsea na Real Madrid, muitaliano Carlo Ancelotti ameelezea tatizo lililopo Chelsea hivi sasa huku akisema kuwa wachezaji wa Chelsea wamekosa morali na kwamba hilo sio tatizo la kocha Jose Mourinho huku akisisitiza kuwa Mourinho ana uwezo mkubwa wa kurudisha hali ya ushindi klabuni.

Carlo Ancelotti maarufu kama King Carlo yupo jijini London ambako alikwenda tangu wiki iliyopita kushuhudia uzinduzi wa filamu ya mchezaji wake wa zamani Cristiano Ronaldo na kufanya mahojiano maalumu na gazeti la Daily Mail la nchini England.

Kocha huyo ambaye amesisitiza ana mahusiano mazuri na kocha Jose Mourinho, ingawa hawajaongea hivi karibuni Ancelotti ametoa siri kwamba kocha huyo alimtumia ujumbe wa kumpongeza mara baada ya kutwaa ubingwa wa kumi wa michuano ya klabu bingwa Ulaya ‘La Decima’.

Akiiongelea klabu ya Chelsea hivi sasa, Ancelloti anasema msimu uliopita klabu hiyo ilitwaa ubingwa kirahisi zaidi nchini England lakini msimu huu wachezaji hawana morali tena ya kujituma. King Carlo anasema ingawa kocha ndiye mwenye jukumu la kuwamotisha wachezaji lakini wakati mwingine ni ngumu kama wachezaji wenyewe hawana nia ya kuwa na morali na kujiamini binafsi.

Ancelotti anaendelea kusema kuwa kocha Jose Mourinho ana uwezo mkubwa sana wa kurudisha hali ya ushindi klabuni hapo na kwamba haitakua busara kumfukuza haraka bila kumpa muda.

Kuhusu kurejea nchini England, King Carlo anasema anaamini ipo siku atafundisha tena nchini England, lakini akasisitiza kuwa hakuwahi kufanya mazungumzo na klabu ya Liverpool kama ilivyokua inaripotiwa.

Kocha huyo ambaye pia amewahi kuifundisha klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, anasema kuwa kitu kimoja klabu ya PSG inakihitaji hivi sasa ni kushinda taji la ubingwa wa Ulaya na kwamba ni kitu pekee alifeli alipokua hapo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here