Home Kitaifa UNAJUA NIDHAMU YA SAMATTA INATOKA WAPI? KWELI MTOTO WA NYOKA NI NYOKA

UNAJUA NIDHAMU YA SAMATTA INATOKA WAPI? KWELI MTOTO WA NYOKA NI NYOKA

509
0
SHARE
Mbwana Samatta (kulia) akilakiwa na babayake mzazi mzee Ally Samatta baada ya kutua uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam
Mbwana Samatta (kulia) akilakiwa na babayake mzazi mzee Ally Samatta baada ya kutua uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam
Mbwana Samatta (kulia) akilakiwa na babayake mzazi mzee Ally Samatta baada ya kutua uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam

Baba mzazi wa Mbwana Samatta mzee Ally Samatta amesema hakuwahi kufikiria hata siku moja kama mwanaye sikumoja angefikia mafanikio ambayo ameyapata akiwa na klabu yake ya TP Mazembe ya nchini Congo DR.

Mtandao huu umefanya mahojiano maalumu na mzee Samatta ili kutaka kujua kama aliwahi kufikiria kama mwanae atakuja kufikia mafanikio aliyonayo leo lakini pia kujua siri ya nidhamu aliyonayo mwanaye inayopelekea kuwa mfano kwa wachezaji wengine wa Afrika.

“Sikutegemea kabisa mpaka juzi alipofunga goli la nane na mpira kumalizika na mchezaji wangu ‘automatically’ akawa mfungaji bora wa Afrika, kuna wimbo niliuimba ambao waliima ‘Marquees’ unaitwa ‘yuko mikononi mwangu’”.

“Nikawa naimba sikutegemea kabisa kitu kama hicho kutokea katika familia lakini namshukuu Mungu kaleta nema yake kijana kafanya maajabu na ndoto imetimia”.

“Kila siku namsisitizia kuwa na nidhamu, mimi na mamayake tulikuwa polisi kila mtu anajua maadili ya polisi, kwahiyo tumemlea kwenye mazingira ya kuwa na nidhamu na nashukuru nidhamu imelala vizuri pale”.

“Huwa namsihi kila anapocheza mpira kama inatokea mtu kakufanyia rafu inamaana kakushindwa, kwahiyo na wewe usimrudishie rafu. Mtu akikufanyia kitu chochote kile katika uwanja inamaana anataka kukutoa kwenye mchezo kwahiyo wewe usicheze nae ila unatakiwa umchunge kwamba ukikutana nae mambo yanaweza kuwa mabaya”.

“Pili namwambia kuhusu waamuzi, nao ni binadamu wanaweza wakaamua lolote uwanjani, kukupa kadi ya njano au nyekundu sasa ili usicheze na marefa, lolote atakaloamua uwanjani wewe kubaliana nalo cheza mpira utakuja kupata mafanikio”.

“Kama mnavyoona akicheza mpira Samatta anaweza akapigwa, akasukumwa lakini yeye akinyanyuka anacheza mpira kwasababu akija nyumbani namfunda. Mimi mwenyewe nilikuwa mchezaji lakini sikupata kadi nyekundu hata mara moja katika uchezaji wangu wa mpira”.

Nataka azidi kusonga mbele kwasababu naona njia anaiona, haya mafanikio ni nusu ya safari yake “.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here