Home Kimataifa UNAHAFAMU TOTTI ALILAZIMIKA KUTOA FEDHA KWA POLISI ILI KUMLINDA MTOTO WAKE

UNAHAFAMU TOTTI ALILAZIMIKA KUTOA FEDHA KWA POLISI ILI KUMLINDA MTOTO WAKE

580
0
SHARE

totti 2Imegundulika kuwa nyota wa klabu ya AS Roma Francesco Totti amekuwa akiwalipa Polisi kwa miaka miwili kuanzia mwaka 2008 na 2010 ili kumlinda mtoto wake wa Kiume Cristian kutoka katika magenge mbalimbali ya uhalifu nchini Italia.

Taarifa za malipo ya mapolisi na kutekwa kwa mtoto wa Totti Cristian zimetolewa na kiongozi wa zamani wa polisi anayefahamaika kama Luca Odevaine wakati akihojiwa na Meya wa mji wa Roma Walter Veltroni juu ya magenge ya uhalifu katika mji wa Roma.

cristian-tottiKatika maelezo yake, Luca Odevaine amesema kuwa “kuna mtu alitolewa gerezani na kupewa kiasi cha euro elfu 50 kwa lengo la kumteka Cristian Totti mtoto wa Francesco Totti”.

Luca anaendelea kwa kusema kuwa “siku moja mwalimu wa mazoezi wa Totti anayefahamika kama Vito Scala alikuja na kunambia kuwa kuna shabiki mmoja wa AS Roma ametoka gerezani hivi karibuni na amepewa kiasi cha euro elfu 50 ili amteke mtoto wa Totti.

Vito akasisitiza kuwa nifuatilie jambo hilo anasema Luca afisa wa zamani wa Polisi.Baada ya hapo Luca alifuatlia hilo jambo na kutoa taarifa kwa mkuu wa kitengo cha usalama kamanda Luongo na pia alimueleza Meya wa jiji la Roma pamoja na idara nyingine za Polisi.

Luca anaendelea kwa kusema kuwa wakati huo bado hakukuwa na uhakika wa taarifa za utekaji wa mtoto wa Totti lakini yeye alilazimika kuwaomba baadhi ya maofisa wa polisi waliokaribia kustaafu kumsaidia Totti kwa kulindia mtoto wake Cristian baada ya muda wa kawaida wa kazi .

totti 1Alichokifanya Totti ni kutoa kiasi cha fedha kwa ajili ya maofisa hao ili ulinzi uwe madhubuti kwa mtoto wake.

Hivi karibuni mji wa Roma umekuwa na matukio mengi yakiharifu yakihusisha uporaji wa kutumia silaha,wizi wa kutumia mitandao katika taasisi mbalimbali za jiji la Roma na mauaji ya raia.

Tayari watu 46wamefikishwa mahakamini kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu katika sehemu mbalimbali za mji wa Roma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here