Home Kimataifa Uchambuzi wa Filamu Cristiano Ronaldo kwenye namba – Rihanna, Man Utd, Madrid,...

Uchambuzi wa Filamu Cristiano Ronaldo kwenye namba – Rihanna, Man Utd, Madrid, Messi wote ndani

822
0
SHARE

Ni siku mbili tangu filamu ya mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo ilipotoka kwa mara ya kwanza na kufanyiwa uzinduzi jijini London – nilipata bahati ya kuitazama filamu hiyo na hapa najaribu kuichambua filamu hii yenye dakika zipatazo 89 kwenye namba na takwimu. Uchambuzi huu unatengeneza taswira ya namna Cristiano alivyotaka kujionesha mbele ya walimwengu.

Ronaldo ametumia dakika 7 na sekunde 28 katika filamu yake kuonyesha akiwa anavaa suit au tuxedo.

Pia ametumia dakika 7:32 akiwa amevaa jezi za Real Madrid.
Supastaa huyo mwenye umri wa miaka 30 amewekeza dakika 3 na sekunde 6 akionekana na timu yake ya taifa ya Ureno, lakushangaza zaidi ameonekana akiitumikia klabu iliyompa umaarufu na kumjenga zaidi Manchester United kwa sekunde 19 tu.

Cristiano Ronaldo pia ametumia dakika 3 na sekunde 45 akiwa hana shati juu ya kiwili wili chake, dakika 2 na sekunde 25 akiwa kwenye ndege binafsi safarini, na dakika 1 na sekunde 7 akiimba wimbo wa Rihanna.

Leo Messi pia ameonekana kwa dakika 2 na sekunde 37.

Jedwali hapo chini linaonyesha vyema mgawanyo wa dakika kwenye filamu hii.

  

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here