Home Ligi EPL SCHWEINSTEIGER AWATULIZA MASHABIKI KUHUSU VAN GAAL

SCHWEINSTEIGER AWATULIZA MASHABIKI KUHUSU VAN GAAL

446
0
SHARE

bastian

Kiungo mkongwe wa Manchester United na timu ya taifa ya Ujerumani Bastian Schweinsteiger amewapa moyo na kuwataka mashabiki wa United wawe wavumilivu dhidi ya kocha wao Louis Van Gaal kutokana na kutofurahia aina ya mpira anaofundisha kocha huyo Muholanzi.

Mara kadhaa sasa Mashabiki wa Manchester United wamekua wakiimba kwa sauti uwanjani ‘Attack Attack Attack’ wakiwataka wachezaji wao kushambulia kwa nguvu kama ilivyokua wakati kocha Sir Alex Ferguson aliyekua akifundisha mpira wa kushambulia muda wote na kupata mafanikio makubwa.

Lakini Bastian Schweinsteiger katika kuwatuliza mashabiki wao amesema, “najaribu kufananisha kinachotokea hapa na kipindi kile tukiwa Allianz Arena na Louis Van Gaal. Ilituchukua muda kama wachezaji kuelewa ni aina gani ya mpira Van Gaal alitaka tucheze. Lakini baada ya muda tulitwaa ubingwa wa ligi huku pia tukifika fainali ya klabu bingwa Ulaya.”

Schweinsteiger amesema kwake yeye hataki kuzungumzia December wala January ila mwezi mei ambapo bingwa ndio anapatikana. Anasema mashabiki wawe wapole na kumuamini kocha Louis Van Gaal kwamba atapata mataji kadri ya muda.

Van Gaal amekua katika kipindi kigumu hivi karibuni baada ya mashabiki na baadhi ya wakongwe wa zamani wa klabu hiyo kama Paul Scholes wakiponda staili yake ya uchezaji kwamba haina tija kwa Manchester United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here