Home Kimataifa SAN ANTONIO SPURS YAWAPIGA WAFALME WA SACRAMENTO

SAN ANTONIO SPURS YAWAPIGA WAFALME WA SACRAMENTO

607
0
SHARE

KAHW

Kawhi Leonard alifunga pointi 24, benchi la San Antonio nalo likazalisha  pointi 24 katika robo ya nne na Spurs ikatoka kifua mbele kwa Sacramento  Kings kwa jumla ya pointi 106-88. Sacramento Kings sasa wamepoteza mchezo wao wa sita mfululizo.

Moja ya maingizo mapya, David West alikuwa na pointi nne katika robo ya nne, pamoja na wachezaji wenzake wa ziada  Boris Diaw na Rasual Butler .

Huu unakuwa msimu wake wa 12 katika ligi ya  NBA. West anadai kuwa anafurahia mtazamo  mzima wa  timu yake huku akisema yote  huanza na kocha Gregg Popovich na pia  uchagizwa na  maveterani wa muda mrefu wa klabu hiyo.

” Sisi hujitahidi kuchukua mbinu bora na nzuri mfululizo na  kila usiku na  hakuna kuachia nafasi katika hilo ,” alisema David West, ambaye alikuwa na pointi nane na rebounds sita . “Kila usiku ni muhimu sana . ”

Tim Duncan alikuwa na pointi 11 na 14 rebounds , LaMarcus Aldridge alikuwa na pointi 16 na rebounds tisa na Tony Parker alikuwa na pointi 13 . Spurs ilipata asilimia 53 ya mitupo waliyorusha.

DeMarcus Cousins  alikuwa na pointi 21 na 12 rebound  katika kurudi kwake kikosini  lakini Kings imepoteza  mchezo wao wa sita mfululizo. Wakiwa na matokeo ya jumla ya 1-7 tangu kuanza kwa msimu, huu unakuwa msimu mbovu na  ni mbaya zaidi kwao tangu msimu wa 1991.

“Nimekuwa katika nafasi ambapo kuna kuanza vibaya. Nimepata kukutana na  kila kitu katika maisha yangu, kutoka michezo sita hadi tisa mfululizo ,” kocha  wa  Kings George Karl alisema. “Kilichopo sasa ni kwa sisi  kucheza zaidi dakika 48 za mpira wa kikapu zinazokuja, mchezo ambao utakuwa  imara zaidi na zaidi yatupasa kucheza  pamoja kama timu. ”

Marco Belinelli alikuwa na pointi 17 na Omri Casspi alikuwa 16 kwa Wafalme. Rajon Rondo alikuwa na pointi 9  na pasi 12.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here