Home Kimataifa NI KIPI KIMEWAKUMBA MEMPHIS GRIZZLIES MSIMU HUU? WAFA KWA L.A CLIPPERS

NI KIPI KIMEWAKUMBA MEMPHIS GRIZZLIES MSIMU HUU? WAFA KWA L.A CLIPPERS

450
0
SHARE

blakeJ.J. Redick alifunga pointi sita mfululizo  katika sekunde za mwisho 55  na kumaliza na pointi 16 na kuisaidia klabu yake ya Los Angeles  Clipppers kuibuka  na ushindi wa pointi 94-92 dhidi ya Memphis Grizzlies Jumatatu usiku.

Los Angeles Clipppers kabla ya mchezo huu walikuwa wamepoteza micheo miwili mfululizo dhidi ya Golden State Warriors na kisha wakafungwa katika mechi iliyokuwa na utata kiasi wa maamuzi dhidi ya Houston Rockets.

“Nahisi tuliufanya  mchezo kuwa mgumu  sana kuliko ilivyotakiwa kuwa ,” alisema DeAndre Jordan , ambaye alikuwa na pointi 13 na 12 rebounds . ” Kuwa na uwezo wa kumaliza mchezo ndo inaonyesha ukomavu wetu . Sidhani kama tungeweza  kuwa washindi wa mchezo huu miaka michache iliyopita. ”

Blake Griffin alikuwa na pointi 24 na 12 rebounds kwa Clippers  katika mchezo huu mgumu uliokuwa wa vuta nikuvute na ambao mpaka mchezo unamalizika hakuna timu iliyopata kuongoza kwa zaidi ya pointi 8.

” Baada ya kuingia na kujikuta katika mchezo wa aina hiyo unachotakiwa kufanya ni wewe kukomaa  tu na kushinda,” kocha wa Clippers Doc Rivers  alisema. “Sisi tulicheza mchezo wao na bahati nzuri tumeshinda lakini si kwamba ndivyo tulivyotaka kucheza. ”

Zach Randolph alifunga pointi 26 kwa Grizzlies , ambayo  imepoteza mchezo wao wa  tatu mfululizo. Marc Gasol aliongeza pointi 18 lakini aliigharimu timu yake kwa kukosa mitupo huru (free throws) nyingi katika sekunde za mwisho mwisho, na Mike Conley alikuwa na pointi 16 .

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here