Home Ligi EPL Gonzalo Higuin kwenda Chelsea? Wakala wake ametoa majibu

Gonzalo Higuin kwenda Chelsea? Wakala wake ametoa majibu

651
0
SHARE

Siku nyingine ya mwezi November imekuja na story nyingine ya usajili barani ulaya.

Story ya leo inaihusisha klabu ya Chelsea – mwandishi wa habari wa Mirror John Cross ameandika habari ambayo anaeleza kwamba mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuin yupo kwenye mipango ya usajili wa dirisha dogo ya klabu ya Roman Abramovich. 

 Higuain ni mmoja wa wachezaji ambao mara zote wamekuwa wakihusishwa na kujiunga na vilabu vya Premier League, lakini kiuhalisia hajawahi kuwa karibu kujiunga na klabu yoyote ya EPL.

Mshambuliaji huyo wa kiargentina kwa sasa yupo kwenye kiwango cha juu katika Seria A, akiwa anaongoza kwa ufungaji wa magoli – magoli 9 katika mechi 12 msimu huu. Story ya Mirror inamuelezea Higuian kama mtu anayekuja kwenye klabu ya Chelsea kuondoa ukame wa magoli baada ya Diego Costa ambaye mpaka sasa ana magoli mawili tu katika mechi 10 za ligi kushuka kiwango – huku akitengeneza vichwa vya habari kwa vitu vya ukosefu qa nidhamu dimbani.

Lakini swali Je Higuain anatajiunga na Chelsea?
Kwa sababu wanazozijua Mirror wameshindwa kuripoti kauli alizotoa wakala wa Higuani – bwana Nicolas Higuian ambaye aliiambia radio ya Crc ya Italia kama ifuatavyo: ‘Miaka mitatu iliyopita Gonzalo alichagua Napoli na unaweza kuona klabu hii inamaanisha nini kwake kwa juhudi anazoonyesha uwanjani.

Ndoto yake, tangu siku ya kwanza alipokanyaga Naples, imekuwa ni kushinda ubingwa wa Scudetto na Napoli. Diego Maradona alishinda Scudetto na Napoli katika msimu wake wa 3 na klabu hiyo na tuna matumaini jambo hilo linaweza kutokea pia msimu na Higuian.’

Higuain ana mkataba na Napoli unaoisha June 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here