Home Kimataifa DAVID MOYES ATUPIWA VIRAGO HISPANIA

DAVID MOYES ATUPIWA VIRAGO HISPANIA

568
0
SHARE

Moyes

Kocha wa zamani wa vilabu vya Manchester United na Everton za nchini England, Mscotish David Moyes amefukuzwa kazi rasmi na klabu ya Real Socieded ya nchini Hispania kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo.

Moyes ambaye alijiunga na timu hiyo mwezi October mwaka jana aliisaidia timu hiyo kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 12 lakini hali imekua ni tofauti msimu huu ambao hadi sasa Real Socieded iko katika hatari ya kushuka daraja kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa katika nafasi ya 16.

Hatua hiyo imekuja siku kadhaa mara baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa Las Palmas huku wakikabiliwa na mechi kati ya bingwa mtetezi wa Europa ligi timu ya Sevilla na baadaye mabingwa wa klabu bingwa Ulaya Barcelona.

Aliyekua kocha msaidizi wa Barcelona ametajwa kuchukua mikoba iliyoachwa na Moyes.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here