Home Dauda TV DAUDA TV: RONALDO AKATAA KUPEANA MKONO NA RAMOS BAADA YA KIPIGO CHA...

DAUDA TV: RONALDO AKATAA KUPEANA MKONO NA RAMOS BAADA YA KIPIGO CHA SEVILLA

521
0
SHARE

Ronaldo vs Ramos

Mambo yanaonekana kutokwenda vyema kunako klabu ya Real Madrid msimu huu. Wana pointi tatu nyuma ya Barcelona katika La Liga, lakini kuna mpasuko mkubwa ambao unaonekana kutokea kunako klabu hiyo iliyo chini ya Mhispaniola Rafa Benitez baada ya kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Sevilla Jumapili iliyopita.

Madrid almaarufu kama Los Blancos walikubali kipigo cha 3-2 kunako dimba la Estadio Ramón Sánchez Pizjuán, huku shukrani za pekee zikienda kwa Ciro Immobile, Ever Banega na Fernando Llorente ambao ndio walipeleka furaha kwa mashabiki wa Sevilla.

Lakini matatizo hayo yanakuja baada ya mfumania nyavu hodari wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo kutoonekana kwenye ubao wa magoli.

Ronaldo amefunga magoli matano tu katika michezo 12 ya mwisho aliyocheza – hali ambayo inampa wakati mgumu sana Mreno huyo huku akionesha kuchukizwa wazi wazi na hali hiyo hasa katika video iliyotoka jana ambayo inamuonyesha akikataa kupeana mkono na beki wa timu hiyo Sergio Ramos baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya mwisho.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here