Home Ligi EPL ARSENAL SASA YAPATA ‘BOOST’ RAMSEY, BELERIN NA OX SHWARI

ARSENAL SASA YAPATA ‘BOOST’ RAMSEY, BELERIN NA OX SHWARI

509
0
SHARE

Arsenal logo

Klabu ya Arsenal sasa imepata ahueni kwa wiki iliyokua mbaya sana kwao baada ya kuandamwa na majeruhi na hata kuwa sababu ya kutopata matokeo katika michezo miwili mfululizo dhidi ya Bayern Munich na Tottenham Hotspur.

Kuelekea michezo ya kimataifa ya kalenda ya FIFA, Arsenal wamepata habari nzuri kutoka kwa wodi yao ya majeruhi baada ya taarifa za kupona kwa winga Oxlade Chamberlain, Aaron Ramsey na mlinzi Hector Bellerin wote kuwa sawa na sasa wanatarajiwa kurudi uwanjani baada ya wiki hii ya kimataifa.

Wachezaji hao ukimtoa Theo Walcott ambaye bado hayuko sawa, wanatarajiwa kupangwa katika mchezo wa ligi kuu nchini humo dhidi ya Westbromwich Albion wiki mbili zijazo.

Taarifa hizi ni nzuri kwa klabu ya Arsenal ambayo wiki mbili zijazo itapigana kugombania nafasi ya kufuzu hatua ya 16 ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, mara baada ya kuwa imeshinda mchezo mmoja tu kati ya minne iliyocheza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here