Home Kimataifa WARRIORS WAO WAENDELEA KUISAKA REKODI, WAITANDIKA DETROIT PISTONS

WARRIORS WAO WAENDELEA KUISAKA REKODI, WAITANDIKA DETROIT PISTONS

435
0
SHARE

curKila mchezaji huwa na siku mbaya. Huu ulikuwa ambao Stephen Curry hakuwa yule aliyezoeleka katika kutupa mitupo yake na kuoatia katika kiwango kizuri tangu msimu uanze. Lakini Golden state Warriors wameedelea kuonyesha kwanini walistahiki kuwa mabingw wa msimu uliomalizika. Hii ni baada ya  kuendeleza rekodi yao ya kutokufungwa na kuwa timu pekee yenye rekodi hiyo mpaka sasa.

Huku Stephen Curry akiwa katika usiku wake mbaya tangu kuanza kwa msimu , Golden State Warriors walipata msaada mkubwa kutoka katika benchi lao yaani wachezaji wa akiba.  Wachezaji hao waliweza kuwasukuma na kuonyesha ni namna gani wamekamilika kama timu na ni bora sana.

Andre Iguodala na Leandro Barbosa  kwa pamoja waliisaidia Golden State jumla ya pointi 23 wakitokea katika  benchi.  Hii iliwasaidia kuanza robo ya nne wakiwa wanaongoza kwa pointi nyingi na kuchangia ushindi wa  kuwapiga Detroit Pistons 109-95, ambayo imeibuka na kuwa moja ya timu ngumu katika NBA siku ya  Jumatatu usiku.

Curry , ambaye alimaliza akiwa na pointi 22, alikosa mitupo mitano kati ya mitupo saba ya kwanza huku  akimaliza kwa kupata mitupo 7 kati ya 18.  Hii ni mara ya tatu pekee tangu mwanzo wa msimu huu kwa Stephen Curry kufunga chini ya point 30. Curry pia alimaliza na pasi 5 na rebound 5.

Klay Thompson aliongeza pointi 24, Barnes alikuwa 12, Iguodala alifunga 13 na Barbosa alikuwa 10, kwa upande wa Golden State Warriors. Rekodi ya 8-0 ni ya pili kwa ubora katika historia ya Golden State Warriors.

Sasa inatakiwa kushinda mchezo mmoja ili kufikia rekodi ya msimu wa 1960-1961, ya kushinda michezo 9 ya kwanza. Rekodi hiyo iliwekwa wakati Golden State Warriors ikifahamika kama Philadelphia Warriors.

Reggie Jackson, akitoka kufunga pointi  40 dhidi ya  Portland ambazo ndio nyingi zaidi katika maisha yake ya NBA, alifunga pointi 20 kwa Detroit ( 5-2 ). Andre Drummond aliongeza pointi 14 na 15 rebound.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here