Home Ligi EPL ZOUMA NAE AIBUKA KUHUSU MOURINHO

ZOUMA NAE AIBUKA KUHUSU MOURINHO

570
0
SHARE

Zouma

Beki wa Chelsea Kurt Zouma amekanusha tetesi zinazodai kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho hana tena sapoti ya wachezaji wake kutokana na muendelezo wa matokeo mabovu ya timu hiyo.

Wikiendi iliyopita Stoke City walipeleka kipigo cha saba kwa wazee hao wa darajani tangu msimu huu uanze, na kuwafanya Chelsea wazidi kuporomoka mpaka nafasi ya 16 wakiwa wamecheza michezo 12 na kujikusanyia kibindoni pointi 11.

Kwa mujibu wa mtandao wa Goal.com, mustakabli wa Mourinho uko mashakani kutokana na kukosa sapoti kubwa ya wachezaji katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Hata hivyo, Zouma amekataa katakata na kusema kwamba wachezaji bado wana imani kubwa na kocha wao, licha ya kushangazwa na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

“Sidhani kwamba ni wachezaji ndio wanaomuwangusha kocha”, Zouma alinukuliwa na Telefoot.

“Hatupo katika kiwango tulichokuwanacho msimu uliopita, lakini bado tupo pamoja kama timu. Bado tuna imani na Mourinho, kama ilivyo kwa upande wa mashabiki.

“Siwezi hata kuelezea majanga haya tuliyonayo. Ni janga kubwa kwa kweli”, aliongeza.

“Tulikuwa mabingwa msimu uliopita…pengine ni tatizo la kisaikolojia”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here