Home Kimataifa STRAMACCIONI KOCHA MPYA PANATHINAIKOS

STRAMACCIONI KOCHA MPYA PANATHINAIKOS

587
0
SHARE

strama 1Kocha wa zamani wa vilabu vya Inter Milan na Udinese Andrea Stramaccioni ametangazwa rasmi kuwa kocha wa klabu ya Panathinaikos ya nchini Ugiriki.

Taarifa hizo zimethibitishwa na klabu ya Panathinaikos na kufuta tetesi zote kuhusu kujiunga au kutojiunga kwa Stramaccioni katika klabu hiyo.

Andrea Stramaccioni amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu akichukua nafasi ya kocha Muingereza Steve Rutter.Stramaccioni amezaliwa tarehe 9/01/1979 akiwa na miaka 39 tu kwa sasa.

essien 2Kocha huyo ataungana na wachezaji wakongwe katika kikosi hicho kama Michael Essien,Mladen Petric na Marcus Berg.

Timu ya Panathinaikos inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya soka nchini Ugiriki ’Super League’ nyuma ya mahasimu wao Olympiakos wanaoshika nafasi ya kwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here