Home Ligi EPL MASHABIKI LIVERPOOL WAMSIKITISHA KLOPP ANFIELD

MASHABIKI LIVERPOOL WAMSIKITISHA KLOPP ANFIELD

602
0
SHARE

Klopp 1

Baadhi ya mashabiki wa Liverpool jana walimuacha peke yake kocha wao Jurgen Klopp mara baada ya mlinzi wa Crystal Palace, Scot Danny kufunga goli la ushindi katika dakika ya 82 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 2-1.

Hicho ni kipigo cha kwanza kwa kocha Jurgen Klopp tangu atue Liverpool hivi karibuni kuchukua mikoba ya Brendan Rogders aliyetupiwa virago mwezi uliopita.

Akielezea tukio hilo mara baada ya mchezo, kocha huyo raia wa Ujerumani alisema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha mashabiki kumkimbia na kumuacha peke yake wakati timu ikihangaika kurudisha bao, hali anayoisema kuwa alijihisi mpweke zaidi na kusikitishwa sana na tukio hilo.

Klopp 2

Klopp amewataka mashabiki kuwa wavumilivu na kwamba haipendezi kutoka uwanjani kabla ya dakika ya mwisho kwani kwenye mpira lolote linaweza kutokea na kwamba ni vizuri kuisapoti timu hadi mwisho.

Aidha katika tukio jingine, Klopp alishuhudia kuumia vibaya kwa mlinzi wake wa kati Mamadou Sakho ambaye leo atafanyiwa scan kuona ni muda gani atakua nje ya uwanja.

Klopp amesema ni heri apoteze mechi hata kwa bao 3-1 kuliko kumpoteza mchezaji kwa majeruhi, kwani kwake mchezaji ndiye muhimu zaidi kuliko matokeo.

Klopp 3

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here