Home Ligi EPL JOSE MOURINHO BADO SALAMA NDANI YA CHELSEA

JOSE MOURINHO BADO SALAMA NDANI YA CHELSEA

562
0
SHARE

Mourinho salama

Pamoja na kipigo cha tatu mfululizo na cha saba tangu kuanza kwa msimu huu, klabu ya Chelsea haina mpango wa kutafuta mbadala wa Mourinho katika wakati huu wa kalenda ya FIFA (International Break) na kwamba Mourinho ataendelea kushika kazi.

Inaelezwa kuwa boss wa Chelsea Roman Abramovic yuko katika mawazo mchanganyiko kuhusu suala la Mourinho na hasa ikizingatiwa kuwa kama watamfukuza Mourinho basi watakua wamemfukuza kocha bora zaidi katika historia ya klabu yao.

Hata hivyo Abramovic amempa nafasi Mourinho kutetea nafasi yake mpaka hapo atakapoona haiwezekaniki basi ataachana na kocha huyo anayepitia kipindi kigumu zaidi katika historia yake ya ukocha.

Lakini habari zisizo rasmi zinasema kuwa huenda kukawa na mahusiano mabovu kati ya Mourinho na mchezaji wake Eden Hazard ambaye amekua akimuweka nje ya uwanja mara kadhaa hivi sasa na hata juzi alipoanza dhidi ya Stoke City hakua na morali ile ile iliyozoeleka tangu msimu uliopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here