Home Ligi BUNDESLIGA HAPPY BIRTHDAY ANDREAS ‘ANDY’ BREHME

HAPPY BIRTHDAY ANDREAS ‘ANDY’ BREHME

629
0
SHARE

andreas brehmeKama umezaliwa leo tarehe 9 mwezi wa 11,basi jua umezaliwa pamoja na mcheza soka wa zamani wa vilabu vya Kaiserslautern,Bayern Munich na Inter Milan Andreas Brehme maarufu kama ‘Andy’.

Andreas Brehme alizaliwa tarehe 9/11/1960.

Andreas Brehme atakumbukwa na mashabiki wengi wa soka baada ya kufunga goli la ushindi kwa Ujerumani Magharibi katika mchezo wa fainali ya kombe la dunia la mwaka 1990 nchini Italia kati ya Ujerumani Magharibi dhidi ya Argentina.

Katika mchezo huo,Ujerumani Magahribi iliibuka na ushindi wa goli 1-0 huku Andreas Brehme akifunga goli kwa njia ya mkwaju wa penati mnamo dakika ya 85 na kuwapa Ujerumani ubingwa wa 3 wa kombe la dunia.

Andreas Brehme hakuishia hapo kwani baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia la 1990, alikuwepo katika kikosi cha Inter Milan kilichotwaa ubingwa wa kombe la UEFA Cup msimu wa mwaka 1990/91 kwa kuifunga AS Roma magoli 2-1.

‘Happy Birthday Andreas Brehme na wote waliozaliwa siku ya leo.’

Angalia goli alillofunga Andreas Brehme katika mchezo wa fainali dhidi ya Argentina 1990.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here