Home Dauda TV DAUDA TV: ANGALIA MAGOLI YOTE YA TP MAZEMBE VS USM ALGER

DAUDA TV: ANGALIA MAGOLI YOTE YA TP MAZEMBE VS USM ALGER

556
0
SHARE

Samatta-celebrates

Jana klabu ya TP Mazembe ilifanikiwa kuifunga timu ya USM Alger kwa bao 2-0 kwenye mchezo wa marudiano wa fainli ya klabu bingwa Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Stade TP Mazembe Lubumbashi, Congo DR.

Mbwana Samatta alifunga goli la kwanza dakika ya 75 kwa mkwaju wa penati baada Roger Assale kuangushwa na beki wa USM Alger kwenye eneo la hatari wakati akielekea kufunga.

Samata alitengeneza goli jingine lililofungwa na Roger Assale dakika ya 90 na kufanikisha ushindi huo wa goli 2-0 dhidi ya USM Alger ya Algeria.

TP Mazembe wakatwaa ubingwa huo kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-1 baada ya mchezo wa awali uliochezwa Algeria kumalizika kwa Mazembe kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here