Home Ligi BUNDESLIGA Ribery anaidai CNN Billion 3.2 – kisa hiki hapa

Ribery anaidai CNN Billion 3.2 – kisa hiki hapa

566
0
SHARE

Winga wa kikataifa wa Ufaransa na klabu ya FC Bayern Munich Frank Ribery amekishtaki kituo cha Television cha Marekani CNN akikidai fidia ya $1.5m sawa na billion 3.2 za kibongo.

  
Ribery amefungua kesi hiyo baada ya kituo hicho cha TV kutumia picha ya mwanasoka huyo katika kuelezea story juu ya matibabu ya cryotherapy – matibabu yanayohusisha kuuweka mwili kwenye sehemu kavu au yenye baridi kali ili kupunguza maumivu au kuponyesha kabisa.

“Mr Franck Ribéry … hakutoa ruhusa ya matumizi ya picha ile kwa kituo cha CNN,” alisema Carlo Alberto Busa ambaye ni mwanasheria wa Ribery wakati akiongea na radio ya Ufaransa – RMC

Picha hiyo ya Ribery ilionekana kwenye akaunti ya Twitter ya CNN na Ribery alionekana kwenye box la cryotherapy huku picha ikisindikizwa na kichwa cha habari kifuatacho: “Mwanamke hakutwa ameganda kwenye box la cryotherapy, matibabu haya yazua maswali.” 

  Busa aliongeza: “Mr Franck Ribéry na familia yake wamenielekeza niende kwenye mahakama nchini Ufaransa kufungua kesi ya kudai fidia isiyopungua $1.5m”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here