Home Ligi EPL ETI PAULISTA ALIKUA HAWAJUI WAPINZANI WAKUU WA ARSENAL

ETI PAULISTA ALIKUA HAWAJUI WAPINZANI WAKUU WA ARSENAL

527
0
SHARE

Paulista

Leo ni siku ambayo mahasimu wawaili wa jiji la London Arsenal na Tottenham wanatarajia kuchuana vikali katika muendelezo wa michuano ya Ligi Kuu nchini Uingereza, lakini jambo la kushangaza ni kwamba kamwe beki wa Arsenal Gabriel Paulista, hakuwa anafahamu kama Spurs ni mahasimu wa Arsenal mpaka alipojiunga na Washika Bunduki hao wa jiji London.

Katika taarifa yake aliyoitoa, Gabriel amesma alijua Chelsea ndio wapinzani wakuu wa Arsenal katika jiji la London.

Aliiambia ArsenalTVHD: “Kujaribu kushinda mechi hizo ni vigumu sana na nadhani mpinzani mkuu ni Tottenham”.

“Watu wanaongea sana kuhusu suala hilo hapa na niliambiwa kuhusu hilo mara tu nilipowasili. Mara zote nilikuwa nikidhani kuwa wapinzani wakuu ni Chelsea, lakini wachezaji wenzangu waliniambia ni Tottenham ndio wapinzani wakuu”.

“Hilo linafanya mchezo huu kuwa mgumu sana”.

Arsenal wana rekodi nzuri sana dhidi ya Spurs wakiwa wameshinda michezo 13 na kupoteza mmoja kati ya michezo ya mwisho 22 ya ligi waliyocheza wakiwa nyumbani dhidi ya Spurs.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here