Home Ligi EPL “NIZOMEENI MIMI, WAACHENI WACHEZAJI”- LOUIS VAN GAAL

“NIZOMEENI MIMI, WAACHENI WACHEZAJI”- LOUIS VAN GAAL

500
0
SHARE

Van Gaal 1

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amewashauri mashabiki wa klabu hiyo kuacha kuwazomea na kuwashambulia wachezaji wake na badala yake amewataka wamzomee yeye kwakua amezoea na kwamba ameshapitia maisha hayo.

Katika mchezo dhidi ya CSKA Moscow Jumanne iliyopita katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya, mara kadhaa mashabiki walilipuka na kuwazomea wachezaji huku wakiimba kuwataka washambulie muda wote kabla ya Wayne Rooney hajafunga goli dakika ya 79 ya mchezo.

Wayne Gaal

Presha ikiwa ni kubwa hivi sasa Old Trafford, mashabiki wanataka kuona mpira wa kushambulia muda wote kama walivyokua wamezoea kwa kocha wao mkongwe Alex Ferguson, lakini Van Gaal anasema muda umefika mashabiki wawe wanachambua mechi na kujua ugumu wa timu wanazokutana nazo.

Kuhusu mechi ya Jumanne dhidi ya CSKA, Van Gaal anasema kuwa amesoma historia na kuona kuwa hata Manchester iliyokua bora zaidi ilishindwa kuwafunga CSKA siku za nyuma lakini sasa anajisikia faraja wameshinda safari hii.

Van Gaal 2

Aidha kuhusu aina ya mpira wanaocheza, Van Gaal anasema anasikia nyimbo za mashabiki wakitaka washambulie, lakini akasema kwa mfano mechi ya Jumanne walishambulia kwa dakika 85 kati ya 90 na kusisitiza kuwa wakati mwingine mashabiki wanatakiwa kujua ugumu wa kucheza na timu zinazozuia dakika zote.

Kuhusu kuzomea zomea, kocha huyo haoni tija ya kuwazomea wachezaji kwani hawana makosa na kwamba inawavuruga kisaikolojia huku akitaka kuzomewa yeye kwani amezoea kwa miaka mingi ya maisha yake ya ukocha.

Young

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here