Home Kimataifa NBA YALA DILI LA MAANA, SASA UNAWEZA KUTIZAMA NBA, WNBA, NA SLAM...

NBA YALA DILI LA MAANA, SASA UNAWEZA KUTIZAMA NBA, WNBA, NA SLAM DUNK KIGANJANI KWAKO

502
0
SHARE

CURRChama cha mpira wa kikapu chini marekani (NBA) kimeingia mkataba wa masoko na biashara na kampuni ya mawasiliano chini humo,Verizon.  Hivyo NBA imekubaliana na kuifanya Verizon kuwa mtoa huduma rasmi wa taarifa za video, dondoo na matukio ambayo yatakuwa yanajiri katika michezo mbalimbali.

VERI

Video hizo zitahusisha  ligi ya wanawake inayosimamiwa na  WNBA, ligi ya kuwaendeleza wachezaji wa yaani  NBA D- League  na timu ya taifa ya mpira wa kikapu( USAB ).

wachezaji wa WNBA, Ellena Della Donne, Maya Moore na Angel Mccoughtry
wachezaji wa WNBA, Ellena Della Donne, Maya Moore na Angel Mccoughtry

Kama sehemu ya ushirikiano mpya , kupitia go90, kutapatikana video za dondoo za yaliyojiri katika NBA, na pia watu wataweza kupata video za yaliyotokea nyuma ya pazia katika michezo mbalimbali kupitia application ya NBA LEAGUE PASS .

legue

Zaidi ya hayo, watumiaji wote go90 watakuwa na fursa ya kipekee ya kuchukua watakayoyapenda katika  NBA na kushiriki na wenzao kupitia (SMS) , Facebook na Twitter.  Katika Taarifa za awali inasemekana dili hili litawaingizia NBA kiasi cha dola za Kimarekani milion 400. Mkataba utakaokuwa wa miaka mitatu.

Verizon itakuwa ndio jina rasmi litakalotumika katika nembo ya  NBA All-Star Slam Dunk . Hii itasomeka kama  ” Verizon Slam Dunk ”  na itatumika mara ya kwanza  katika mashindano ya  NBA All-Star 2016  katika jimbo la Toronto.

Verizon itatumika kutangaza na  kuwa mshirika wa programu ya kupiga kura kwa ajili ya NBA All-Star. Ni rasmi kuwa Verizon itakuwa mshirika wa  NBA Draft , NBA Summer League  na Jr. NBA.  Mwanzo wa msimu wa 2016, Verizon itakuwa mshirika rasmi wa ligi ya wanawake yaani WNBA.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here