Home Kimataifa Hii ndio kauli iliyomtia hatiani Benzema kwenye kesi ya mkanda wa ngono...

Hii ndio kauli iliyomtia hatiani Benzema kwenye kesi ya mkanda wa ngono wa Valbuen

907
0
SHARE

Karim Benzema yupo kwenye matatizo ya makubwa ya kisheria hivi sasa.

  Pamoja kesi ya traffic ambayo inaweza kumpeleka kizimbani siku ambayo kutakuwa na El Clasico, mshambuliaji wa Real Madrid amejikuta kwenye mkono aa sheria tena katika kesi ya blackmail dhidi ya mwanasoka mwenzie wa kifaransa Mathieu Valbuen. 

Benzema ametuhumiwa na sasa amefunguliwa kesi ya kushiriki kujipatia kipato isivyo halali dhidi ya Valbuena, na kushirikiana na kundi la wahalifu katika kesi hiyo. 

Kundi hilo la uhalifu lilikuwa na mkanda wa ngono ambao Valbuena nae alishiriki; wakatishia kuuanika mkanda huo kama Valbuena hatolipa kiasi fedha kwao. 

  Mwanasheria wa Benzema amekaririwa akisema kwamba mteja wake alikuwa akijaribu kunsaidia rafiki kuondokan na jambo hilo, lakini kesi imemkalia vibaya Benzema. 

Mtandao aa habari wa kifaransa aa m6 umetoa kauli ya Benzema iliyorekodiwa kupitia simu aliyokuwa akizungumza na wahalifu. 

Kwenye sauti hiyo Benzema anasikika akisema: ‘Msijali, hana namna ya kutoka kwenye hili. Nitamshawishi afikirie upya na atawalipa tu.’ 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here